Kijiji cha Ngareni Rombo Chaomba Umeme

WAKAZI wa Kijiji cha Ngareni Kata ya Ngoyoni Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wameliomba Shirika la Kusambaza Umeme (TANESCO) kupelekewa huduma ya umeme jambo ambalo linawasababishia kuzorota kwa maendeleo katika kijiji hicho. Diwani wa Kata hiyo Protas Lyakurwa Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wakati alipokua akichangia taarifa ya Shirika la kusambaza umeme iliyowasilishwa na Meneja wa TANESCO, Wilaya …

Mbunge Chadema Alia na Itikadi

MBUNGE wa Jimbo la Rombo, Joseph Selasini amewataka wakazi wa Wilaya ya Rombo kuweka pembeni itikadi zao za kisiasa na badala yake kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ili waweze kuleta maendeleo. Mbunge aliyasema hayo wakati alipokuwa akihutubia wakazi wa Kata ya Mrao Keryo, Tarafa ya Mashati Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro. Amewataka wananchi kuacha tabia ya kukaa vilabuni na kunywa pombe …

Aliyebaka Mwanafunzi Darasa la Nne Ahukumia Miaka 30

Yohane Gervas, Rombo MAHAKAMA ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha miaka 30, Philipo Mbiti (38) baada yakupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la nne. Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Rombo, Naomi Mwerinde alisema mahakama imemtia hatiani baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, ambapo upande wa mashtaka umedhibitisha …

Mtoto Amuua Baba Yake kwa Rungu

MTU mmoja mmwenye umri kati ya 65-70 ameuawa baada ya kupigwa na Rungu kichwani na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wake, Mkazi wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro. Ofisa Mtendaji wa Kijiji Cha Ikuini, Gaspar Kauki amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba limetokea mnamo Agosti 8, mwaka huu majira ya saa nne usiku katika kitongoji cha Imongoni Kijiji cha …

Waliouwa kwa Deni la Shs 9600 Wanyongwa Rombo

WATU watatu wakazi wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wamehukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mauaji. Hukumu hiyo imetolewa jana Mahakama Kuu Kanda ya Moshi iliyokuwa ikiendesha vikao vyake katika Mahakama ya Wilaya ya Rombo chini ya Jaji Amaisario Munisi. Awali kabla ya kusoma hukumu hiyo, Mwanasheria wa Serikali, Tamari Mndeme aliwataja watuhumiwa …

TASAF Kupunguza Umaskini Kwenye Familia Rombo

Yohane Gervas, Rombo MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), imedhamiria kupunguza umasikini katika familia kupitia mpango wa kunusuru hali ya umasikini kwenye kaya unaotekelezwa na mfuko huo katika awamu ya tatu. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa uwezeshaji wa Mafunzo TASAF, Fariji Michael, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Ladislaus Mwamanga, kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tano ya kuwajengea …