Paka Amponza Mfugaji, Amfunga Miaka 3 Jela

MAHAKAMA ya mwanzo Mengwe wilayani Rombo imemhukumu mkazi wa Rombo, Godfrey Kimaryo(32) kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya shambulio la mwili kwa kumjeruhi vibaya mtoto wa miaka tisa kwa madai kua aliiba paka wake. Hukumu hiyo imetolewa na hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mengwe, Adinani Kingazi kesi ambayo ilivuta hisia za watu wengi …

Wanafunzi wa Awali Tunduru Wasomea Chini ya Mti

Na Joachim Mushi, Tunduru WANAFUNZI wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wanasomea chini ya mti kutokana na darasa hilo kuendeshwa bila ya kuwa na chumba maalum kwa ajili ya kusomea wanafunzi hao. Hali hiyo imebainika baada ya mwandishi wa habari hizi kuitembelea shule hiyo hivi karibuni na kuwakuta wanafunzi wakiwa wamekaa chini …

Waziri Pinda Asuluhisha Mgogoro Kiwanda cha Chai Mponde

*Ataka iundwe timu ya watu wachache kusimamia kiwanda   WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amewataka Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai pamoja na Bodi ya Chai nchini waangalie uwezekano wa kuunda timu ya watu wawili au watatu itakayosimamia mwenendo wa kiwanda cha chai Mponde, kilichopo wilayani Lushoto mkoani Tanga.   Waziri Mkuu ambaye aliwasili jijini Tanga Septemba 13, 2014 …

Mtoto wa Chekechea na Kaka Yake Walawitiwa

*Mlezi wao bibi miaka 80 aomba asaidiwe kisheria Na Yohane Gervas, Rombo WATOTO wawili wa Kijiji cha Aleni Chini, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, mmoja akiwa na umri wa miaka 9 na mwingine miaka 6 wote wanafunzi Shule ya Msingi Aleni (majina tunayo) wanadaiwa kulawitiwa na mtu mmoja mkazi wa kijiji hicho. Akizungumzia Tukio hilo Mkuu wa Shule ya Msingi …

Mbunge Awataka Wananchi Kuacha Kilimo na Kufuga Nyuki

Na Yohane Gervas, Rombo WANANCHI wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wametakiwa kupanda miti na kujishugulisha na ufugaji wa nyuki na kuacha kulalamikia wanyama pori aina ya nyani na temba wanaoharibu mazao ya mahindi. Hayo yalisema jana na mbunge wa jimbo hilo Joseph Selasini, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ushiri wilayani humo, ambapo alisema ni vyema wananchi wakajishugulisha na …

Madiwani Rombo Wambana Mkurugenzi

Na Gelvas Yohane MADIWANI wa Wilaya Rombo mkoani Kilimanjaro wamemtaka Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje kutoa ufafanuzi juu ya fedha zaidi ya shilingi milioni 46 zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa kiwanda cha maziwa na ufugaji wa samaki. Wakizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wametaka kupewa taarifa kwanini tangu fedha hizo kutengwa mwaka 2006 hakuna kinachoendelea. Diwani …