Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo Mei 19, 2016 imetinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini katika mfululizo wa michuano maalumu ya kimataifa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16). Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa …
Erasto Nyoni Aliiponza Azam Kupokwa Pointi
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepitia marejeo ya uamuzi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) kuipoka pointi zake ilizovuna kutoka mchezo Na. 156 dhidi ya Mbeya City ya Mbeya katka mchezo uliofanyika Uwanja wa sokoine mjini Mbeya. Katika Kamati Maalumu ya TFF iliyoketi ndani ya saa 72, chini ya sekretarieti ya TFF na Bodi ya Ligi, iliyoketi Mei …
TFF Yaweka Mitego Kwa Wapanga Matokeo Ligi Kuu
Wakati pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara likitarajiwa kufungwa Jumapili Mei 22, 2016 kwa michezo minane, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa onyo kali kwa timu zote kutojiingiza kwenye mtego wa aina yoyote wa kupanga matokeo. Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameziasa timu zote za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kucheza mechi hizo kwa kufuata taratibu, kanuni …
Liverpool Yaangukia Pua Kwa Sevilla
Klabu ya Liverpool baada ya miaka mingi bila kuingia hatua ya fainali michuano ya Europa Ligi Leo Imeambulia kichapo cha bao 3-1 katika fainali dhidi ya Sevilla Liverpool ndio walikua wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Sturridge dakika ya 35 kabla ya sevilla kusawazisha sekunde chache timu hizo zilipotoka mapumziko kupitia kwa Kevin Gameiro, kabla ya Coke …
Maandalizi Fainali Kombe la Shirikisho Sio Mchezo
Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zitakazokutanisha timu za soka ya Young Africans na Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa zitafanyika Mei 25, 2016 kama ilivyotangazwa awali. Awali fainali hizo zilipangwa Juni 11, 2016 ili kuzipa muda wa kuajindaa timu mara baada ya michezo ya mwisho ya Ligi Kuu ya …
Azam Waachana na Stewart Hall
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, leo imeachana rasmi na aliyekuwa Kocha Mkuu wake, Stewart Hall, baada ya kufanyika makubaliano ya pande zote mbili. Uongozi wa Azam FC umechukua hatua hiyo kufuatia hivi karibuni Hall kutangaza uamuzi wa kuachia ngazi akiweka wazi kuwa amechoka kufundisha soka Tanzania na sasa anataka kwenda kutafuta changamoto nyingine mpya ya kufundisha …