Airtel Kuinua Michezo Kwa Vijana wa Tanzania

Kampuni ya Airtel Tanzania jana Ijumaa Mei 20, 2016 imekutana na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kuzungumzia mipango ya maendeleo wa mpira wa miguu nchini ikiwa ni pamoja na michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu. Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine ambaye ndio aliongoza kikao hicho, alitoa shukrani ka kampuni …

Ligi Kuu Tanzania Bara Kumalizika Kesho

Michezo ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili, Mei 22, 2016 kwa timu zote 16 kutinga katika viwanja vinane tofauti kumaliza ngwe ya msimu wa 2015/16. Michezo itakayopigwa kesho ni pamoja na Simba itakayokipiga na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC ambayo inawania nafasi ya pili kama Simba, …

Aliyekua Rais wa Soka la Ujerumani Kupigwa Jela Miaka Miwili

Jopo la maamuzi la Kamati ya maadili ya FIFA limependekeza kuwa aliyekuwa rais wa Shirikisho la soka nchini Ujerumani – DFB Wolfgang Niersbach apigwe marufuku ya kujihusisha na shughuli zozote za kandanda kwa miaka miwili Hatua hiyo ni kuhusiana na kashfa inayozunguka kibali cha nchi hiyo kuandaa Kombe la Dunia mwaka wa 2006. Niersbach, makamu wa rais wa kamati iliyoandaa …

Serengeti Boys Kukipiga Kesho na Malayasi

Timu ya Taifa ya vijana wa Tanzania wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys siku ya Jumamosi itacheza na Malaysia kwenye mechi yao ya mwisho ya kundi wakisaka ushindi ili kutinga fainali ya 2016 AIFF Youth Cup huko Tilak Maidan Stadium, Vasco, Goa nchini India. Tanzania mpaka sasa imeshacheza mechi 3 na kuifunga India 3-1 na kutoka Sare na USA …

Azam Sasa Mambo Safi, Wahispania Washika Usukani

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, tayari umefikia makubaliano na wakufunzi kutoka nchini Hispania, Kocha Mkuu Zeben Hernandez na Mtaalamu wa Viungo, Jonas Garcia. Makocha hao wawili waliotua nchini Ijumaa iliyopita, kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao wakirithi mikoba ya Mwingereza Stewart Hall, aliyeachia ngazi pamoja …

Mchina Ainunua Klabu ya Aston Villa

Klabu ya soka ya Aston villa ambayo imeteremka daraja msimu huu katika ligi kuu ya England,hatimaye imenunuliwa na tajiri wa kichina Tony Xia ambaye ni mfanya biashara aliyewekeza katika sekta ya Michezo,Utalii,kilimo na afya. Xia ameinunua Aston Villa kwa gharama ya dola milioni tisini (90), amesema amekuwa ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo kwa miaka mingi ingawaje hajafurahishwa na matokeo …