Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani. Klabu hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200. Mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina alifunga mabao 18. Rais wa Indi Native Diego Culequi amesema matokeo …
Uchanguzi Yanga Umepamba Moto
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza leo Mei 27, 2016 kuanza kwa mchakato wa kuchukua fomu za kugombea uongozi katika Klabu ya Young Africans ya Dar es Salaam inayotarajia kufanya uchaguzi tarehe 25 Juni mwaka huu. Nafasi zinazogombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanane wa Kamati ya Utendaji. Kwa …
Michael Wambura Apata Dili CAF
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016. Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. …
Tanzania Yajitoa Kuandaa Michuano ya CECAFA
Shirikisho a Soka Tanzana (TFF), limetangaza kutoandaa michuano ya kuwania Kombe la timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama ilivyopendekezwa. Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa. Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua …
Stars Kuondoka Kesho Kwenda Kuivaa Harambee Stars
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho saa 12.00 alfajiri kwenda Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa. Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa …
Azam Fc Yakiona Cha Moto Taifa, Yachapwa na Yanga
Klabu Azam imeambulia kichapo cha bao 3 – 1 dhidi ya Yanga sc na kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. AmissiTambwe mbao mawili na goli la tatu likifungwa na Simon Msuva lile la Azam likifungwa na Didier Kavumbagu