FAINALI LIGI YA TAIFA KESHO

LIGI ya Taifa hatua ya fainali inaanza Agosti 6 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, ikishirikisha timu 12 zilizogawanywa katika makundi matatu ya timu nne. Timu ya kwanza kutoka kila kundi na washindwa bora wawili (best losers)- watafanya jumla ya timu tano zitakazopanda Daraja la Kwanza. Kundi A lina timu za Polisi Morani (Arusha), Mgambo Shooting (Tanga), Samaria …

KOZI YA MAKAMISHNA WA MPIRA WA MIGUU

KOZI ya makamishna wapya kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Taifa na Kombe la Taifa itafanyika ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Agosti 6-8 mwaka huu. Kwa wanaotaka kuwa makamishna ni lazima washiriki katika kozi ambapo ada ni sh. 10,000. Washiriki wanatakiwa kuwa waamuzi wastaafu na viongozi (administrators) wa mpira …

Azam FC ziarani Uganda, Rwanda

TIMU ya Azam FC inatarajia kuondoka Jumatatu mchana na ndege ya Shirika la Ndege la Uganda kuelekea nchini Uganda na baadae Rwanda kukamilisha ziara yake ya maandalizi ya Ligi Kuu (VPL) inayotarajia kuanza August 20 mwaka huu. Azam itaondoka baada ya kumaliza mchezo wa mechi ya kirafiki kati yake na timu ya Polisi Dodoma inayotarajia kufanyika Jumamosi ya Agosti 6, …

RUFANI YA SHINYANGA UNITED YATOLEWA UAMUZI

KAMATI ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mstaafu Alfred Tibagana imekutana leo kusikiliza mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa mbele yake. Shinyanga United ilikata rufani kupinga kuenguliwa kwenye fainali hizo, uamuzi uliofanywa na Kamati ya Mashindano ya TFF baada ya klabu hiyo baada ya kutozingatia maelekezo ya TFF …

Poulsen awaita 20 kuunda Stars

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ugenini inayochezwa kwenye tarehe zinazotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA dates. Mechi itachezwa Agosti 10 mwaka huu. Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa; Shabani Dihile (JKT Ruvu) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa …

Taswa waandaa bonaza la michezo miaka 50 ya uhuru

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimeandaa bonanza maalum la kuwapongeza wanamichezo mbalimbali waliopata kuiletea sifa nchi katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Bonanza hilo litafanyika jijini Dar es Salaam Novemba 5, 2011 mahali patakapotangazwa, ikiwa ni kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 9, 2011. Kikao …