Azam FC yatoka suluu na SC Villa ya Uganda

Kampala, TIMU ya Azam FC imetoka sare na Timu ya Mpira wa Miguu ya SC Villa ya nchiniUganda. Katika mchezo huo uliochezwa jana mjini Kampala, Azam ilicheza mpira mzuri uliowavutia na kuwaacha na mshangao mkubwa Waganda. Azam FC katika mchezo huo imefanikiwa kutoka sare ya 0-0 na wenyeji SC Villa katika mchezo mkali wa kuvutia uliochezwa kwenye uwanja mkongwe wa …

TFF yatupilia mbali pingamizi la Yanga dhidi ya Simba

KAMATI haikusikiliza pingamizi la Yanga dhidi ya Simba kuhusu wachezaji iliyotoa kwa mkopo baada ya kubaini kuwa wachezaji ambao Simba imewatoa kwa mkopo ni wane tu; Haruna Shamte (Villa Squad), Aziz Gilla (Coastal Union), Ahmed Shiboli (Kagera Sugar) na Mohamed Kijuso (Villa Squad). Wachezaji wengine waliotajwa na Simba kupelekwa kwa mkopo katika klabu mbalimbali ilibainika kuwa ni wa kikosi cha …

MECHI YA STARS, SUDAN YAFUTWA

CHAMA cha Mpira wa Miguu Sudan (SFA) kimefuta mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na timu ya Taifa ya nchi hiyo ‘Nile Crododile’ iliyokuwa ichezwe Agosti 10 mwaka huu. Uamuzi huo umetokana na wakala wa mechi hiyo Hadi Sharkawy kushindwa kupata kwa wakati tiketi ya kuisafirsha Taifa Stars kwenda Khartoum. Pia kutokana na mechi hiyo kufutwa, kambi ya Stars …

JAN POULSEN AONGEZA WAWILI STARS

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewaita kwenye kikosi hicho wachezaji Juma Jabu kutoka Simba na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ wa Azam FC kwa ajili ya mechi ya kirafiki inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana mjini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura ni kwamba; wachezaji hao …

SERENGETI BOYS WAITWA MAZOEZINI

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Kim Poulsen na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo wameita wachezaji 37 kwa ajili ya mazoezi kujiandaa kwa michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Michuano hiyo imepengwa kufanyika Nairobi, Kenya mwishoni mwa mwezi huu ingawa bado CECAFA haijatoa …

Nyota wa soka Japan Naoki afariki dunia

MCHEZAJI Kandanda wa Japan, Naoki Matsuda amefariki dunia siku mbili baada ya kupoteza fahamu uwanjani akiwa mazoezini huku ikiaminika kifo chake kimetokana na maradhi ya moyo. Matsuda (34), aliyeiwakilisha Japan katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2002, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumanne baada ya tukio la kuanguka akiwa mazoezini. Alikuwa akifanya mazoezi na klabu yake ya Matsumoto Yamaga, …