Timu ya Kamanda Kova yaingia Daraja la Kwanza

Na Mwandishi wetu’ LIGI ya Taifa ngazi ya Fainali imemalizika jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga, huku ikizipa nafasi ya kupanda daraja la kwanza timu za Polisi Central ya Dar es Salaam, Mlale JKT ya Ruvuma na Mgambo Shooting ya Tanga. Timu zingine zilizofanikiwa kupanda daraja kama washindwa bora ni Samaria ya Singida na Small Kids ya Rukwa. Taarifa …

Kuziona Simba na Yanga Jumatano sh 5,000/-

Na Mwandishi Wetu, VIINGILIO katika mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya mabingwa watetezi Yanga na Makamu Bingwa Simba itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu kuanzia saa 2.00 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni kama ifuatavyo vitaanzia sh. 5,000 na kuendelea. Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam, …

Newcastle, Arsenal watoka sare, Bolton yauwa, Leverpool yakwama

NEWCASTLE imetoka sare ya 0-0 na Arsenal katika mchezo uliokuwa na kasoro za hapa na pale. Katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal kutoka Ivory Coast, Gervinho alioneshwa kadi nyekundu baada ya kushikana mashati na Joey Burton wa Newcastle. Awali Burton alikanyagwa kwa makusudi na Alex Song, ingawa mwamuzi hakuona tukio hilo. Arsenal licha ya kujaribu kucheza mtindo wao wa ‘kuteleza’ …

Usajili Ligi Daraja la Kwanza Agosti 17

USAJILI wa wachezaji wa klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu huu utafanyika baada ya kumalizika Ligi ya Taifa hatua ya fainali inayoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga. Baada ya fainali hizo kumalizika Agosti 14 mwaka huu TFF itatoa mwelekeo wa usajili huo (roadmap) ikiwemo tarehe ya kuanza na kumalizika, pamoja na kipindi cha pingamizi. Timu …

Kamati TFF yamrejesha Mchaki

KAMATI ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Agosti 10 na 11 mwaka huu kujadili rufani ya Frank Mchaki kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kumuengua kugombea nafasi ya Katibu Mkuu katika uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA). Chini ya Mwenyekiti wake Deogratias Lyatto, Kamati …

Simba na Yanga sasa kuvaana usiku Agosti 17

MECHI ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya mabingwa watetezi Yanga na Makamu Bingwa Simba itachezwa usiku (Agosti 17 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Dar es Salaam na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, uamuzi wa mechi hiyo kuchezwa usiku kuanzia …