Robin van Persie nahodha mpya Arsenal

MSHAMBULIAJI wa Arsenal Robin van Persie amethibitishwa kuwa nahodha mpya wa klabu hiyo. Mshambuliaji huyo (28) anayechezea pia timu ya taifa ya Uholanzi, amekuwa katika klabu ya Arsenal tangu Mei, 2004 na anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Cesc Fabregas, aliyehamia klabu ya Barcelona wiki hii. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema; “Van Persie ni kiongozi kutokana na uchezaji wake, kutokana …

Gervinho wa Arsenal afungiwa mechi tatu

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Gervinho Kouassi amefungiwa mechi tatu kufuatia kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya soka ya England msimu huu dhidi ya Newcastle. Gervinho alitolewa baada ya kushikana mashati na Joey Barton, ambapo kiungo huyo wa Newcastle alianguka uwanjani. Arsenal walikata rufaa kupinga kufungiwa kwa mechi tatu kutokana na sheria zinavyosema mchezaji akioneshwa …

GERVAIS ANOLD KAGO KUNG’ARA NA SIMBA LIGI KUU YA VODACOM

Simba imeingia mkataba na mchezaji Gervais Anold Kago kutoka klabu ya Olympic Real de Bangui ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa. Akiyasema hayo Alex Mgongolwa ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya Sheria , Maadili na Hadhi za wachezaji amesema “Wakati Kago akiwa bado hajapata Hati …

Ligi kuu ya England Sergio Aguero aanza vyema.

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini, amemfananisha Sergio Aguero sawa na mshambuliji wa zamani wa Brazil Romario, baada ya Muargentina huyo kuanza vyema katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea. Aguero aliyenunuliwa kwa kitita cha paundi milioni 38 alifunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa jingine, wakati Manchester City ilipoibuka kwa ushindi wa mabao …

Hatimaye Febregas atua Barcelona

Cesc Fabregas tayari ni mchezaji rasmi wa Barcelona baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ulaya. Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal amefuzu uchunguzi wa afya yake aliofanyiwa mara mbili siku ya Jumatatu katika hospitali iitwayo Hospital de Barcelona, na atatambulishwa na klabu hiyo wakati wowote. Arsenal itapokea kitita cha paundi milioni 30 na paundi milioni …

Nyota wa mpira wa kikapu Marekani kuja Tanzania

Taarifa kwa wadau na wapenzi wa mpira wa kikapu Tanzania. SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania pamoja na ndugu zetu wa Ubalozi wa Marekani nchini tuna furaha kubwa leo kwa mara nyingine tena kufanikisha ziara ya kimichezo ya mafunzo ya wachezaji wa zamani wa ligi kubwa ya mpira wa kikapu duniani ya NBA na WNBA. Miongoni mwa wachezaji wanaokuja katika …