African Lyon kuwalipa Komba, Masenga kwa viingilio

Na Mwandishi Wetu TIMU ya African Lyon imeomba kuwalipa kwa makato ya mlangoni wachezaji wake wawili wanaoidai; Godfrey Komba na Abdul Masenga ambao ilikatiza mikataba yao msimu uliopita. Awali Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliiagiza Lyon kuwalipa wachezaji hao kufikia Agosti 17 mwaka huu vinginevyo isingeruhusiwa kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom iliyoanza leo, Agosti 20 mwaka huu. …

Timu washiriki Ligi Kuu kulamba mil 26.3 kila moja

Na Mwandishi Wetu KILA timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajia kupewa jumla ya sh. milioni 26.3, fedha zitakazotumika kama gharama ya klabu katika mashindano hayo. Akizungumza na vyombo vya habari jana Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema fedha hizo zitatolewa kwa awamu tano tofauti kuanzia mwezi huu. Aidha Wambura alisema kwa Agosti kila timu …

Msimu mpya Ligi Kuu kuanza kesho, timu 10 kupambana

Na Mwandishi Wetu MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/12 unaanza kesho, Agosti 20 mwaka huu, ambapo timu 10 kati ya 14 zinazoshiriki katika ligi hiyo zitakuwa viwanjani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Dar es Salaam na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amezitaja mechi za kesho ni pamoja na Coastal Union Vs Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga), Kagera …

Stars, kuikaribisha Algeria Mwanza

MECHI ya mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) itachezwa Septemba 3 mwaka huu jijini Mwanza.   Bonifase Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amesema leo …

Uefa wamkalia kooni Wenger

ARSENE Wenger huenda akakabiliwa na hatua zaidi za nidhamu kutoka Uefa baada ya kuthibitishwa mawasiliano yake na benchi la ufundi la Arsenal yanachunguzwa. Wenger alikuwa akitumikia adhabu ya kutokaa kwenye benchi la timu hiyo wakati wa mechi ya kufuzu kwa Ubingwa wa Ulaya dhidi ya Udinese. Arsenal ilikuwa inahisi Wenger huenda angeruhusiwa kupitisha ujumbe kwa msaidizi wake Pat Rice kwa …

Breaking Newz, Simba wapeleka kilio Jangwani, waikung’uta Yanga 2-0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam HADI pambano la ngao ya hisani kati ya Simba na Yanga linalofanyika katika uwanja wa taifa Dar es Salaam matokeo ni kwamba, Simba inaongoza kwa mabao mawili kwa bila (2-0). Haruna Moshi ndiye wa kwanza kuifungia Simba katika dakika ya 16 huku Felix Sunzu akiongeza goli la pili katika dakika 38. Mpira sasa ni …