Yanga, Simba zabadili viwanja Ligi ya Vodacom

Na Mwandishi Wetu TIMU za Simba na Yanga zote za jijini Dar es Salaam zimefanya mabadiliko ya viwanja zitakavyovitumia katika Ligi Kuu ya Vodacom baada ya Serikali kuufunga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao ulikuwa utumiwe na timu hizo. Marekebisho hayo yametolewa leo na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es …

TFF yawashtaki Rage, Sendeu Kamati ya Nidhamu

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepeleka mashtaka mbele ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu. Taarifa hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura na kuongeza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada …

Yanga yachezea kichapo tena, Simba yatafuna tena

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam jana imeendelea kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kujikuta ikifungwa tena na Timu ya JKT Ruvu kwa bao moja kwa mtungi. Yanga ambayo jana mjini Morogoro ilionekana kucheza kwa kuzidia karibuni muda wote wa mchezo, ilijikuta ikifungwa goli moja kwa njia ya penati baada ya mmoja wa washambuliaji …

Timu ya Soka ya ‘Bongo Starz’ yaendelea na mazoezi! Pt 2

Na Mwandishi Wetu, Los Angeles TIMU ya Watanzania waishio Kusini mwa California jana Jumamosi walikutana kwa mara nyingine tena, kwa ajili ya mazoezi kabla ya mechi za mataifa mbalimbali kuanza hapo September 3, 2011 na kumalizika tarehe hiyohiyo. Mashindano hayo yatafanyika jijini Los Angeles, California.  dev.kisakuzi.com, ilikuwepo uwanjani kushiriki na pia kushuhudia jinsi timu ilivyokuwa inafanya mazoezi ya nguvu katika upande …

Timu ya Soka ya ‘Bongo Starz’ yaendelea na mazoezi! Pt 1

Na Muandishi wetu, Los Angeles Timu ya Watanzania waishio kusini mwa California jana Jumamosi walikutana kwa mara nyingine tena, kwa ajili ya mazoezi kabla ya mechi za mataifa mbalimbali kuanza hapo September 3, 2011 na kumalizika tarehe hiyohiyo. Mashindano hayo yatafanyika jijini Los Angeles, California.  dev.kisakuzi.com, ilikuwepo uwanjani kushiriki na pia kushudia jinsi timu ilivyokuwa inafanya mazoezi ya nguvu katika upande …

Fifa yaruhusu ITC ya Kago itolewe

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeruhusu Shirikisho la Mpira wa Miguu Jamhuri ya Afrika ya Kati kutoa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa mchezaji, Gervais Anold Kago aliyejiunga na timu ya Simba kutoka Olympic Real de Bangui ya huko. Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na TFF leo, FIFA imeruhusu ITC itolewe baada …