Na Muandishi wetu, Los Angeles Timu ya Soka ya Watanzania waishio Los Angeles, “Bongo Starz” walikutana kwa mara nyingine tena jana siku ya Jumamosi kwa mazoezi ya nguvu kabla ya mpambano wa timu za Afrika kufanyika Septemba 3. Timu ya Tanzania (Bongo Starz) ipo ndani ya kundi C, ambalo linajumuisha timu za Ivory Coast na Ghana. Timu ya Tanzania ni ngeni …
Wachezaji 20 Twiga Stars kwenda maputo
TIMU ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inatarajia kuondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu. Twiga Stars katika msafara wake itakuwa na jumla ya watu 20 ambapo kati yao 16 ni wachezaji na wanne ni viongozi wakiwemo Kocha Mkuu Charles Boniface …
Poulsen awaita 12 kuivaa Algeria
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen jana, Agosti 25 ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo dhidi ya Algeria ‘Desert Warriors’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon. Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). …
Uholanzi yaipiku Hispania ubora wa soka
Uholanzi imeipiku Hispania katika nafasi ya kwanza ya ubora Fifa wa kusakata soka duniani, huku Englan ikipanda nafasi mbili juu hadi ya nne. Wachezaji wa Uholanzi Hispania mabingwa wa soka duniani na Ulaya, wameporomoka hadi nafasi ya pili baada ya kupoteza pointi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia. England, licha ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Uholanzi kuahirishwa, …
Nasri rasmi kukiputa Man City
Manchester City wamekubaliana na Arsenal kumsajili kiungo Samir Nasri. Nasri sasa anaelekea mjini Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya. Nasri alifanya mazoezi na Arsenal siku ya Jumanne asubuhi kujiandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Udinese, utakaochezwa Jumatano. Hata hivyo jina lake liliondolewa kwenye orodha ya wachezaji. Kiungo huyo kutoka Ufaransa anakwenda Manchester pia kukamilisha mkataba wake …
Leseni ya Castory Mumbara yakwama TFF
Na Joachim Mushi TFF imeshindwa kumpa leseni Castory Mumbara ambaye ameombewa usajili katika timu ya Toto Africans kutokana na kutokuwa na Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC), ambayo inatakiwa kutolewa kupitia mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS). Taarifa hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na TFF, kupitia kwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura alipokuwa akizungumza na vyombo vya …