TIMU ya wanawake ya Taifa ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza mechi yake ya kwanza ya michezo ya All Africa Games (AAG) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Ghana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machava, jijini Maputo. Kwa mujibu wa Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis hadi mapumziko timu hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Mwanahamisi Shuruwa aliisawazishia Twiga Stars …
Bongo Starz yaichapa Ivory Coast bao 4 kwa 1!
Na Mwandishi Wetu, Los Angeles, CA ILE siku ya Septemba 3, ambayo ilikuwa ikisubiriwa na wa-Afrika wengi hapa jijini Los Angeles iliwadia. Timu 24 za mataifa ya Kiafrika zilikutana kwa ajili ya kuchuana kwenye mpira wa miguu, ambao mshindi alijinyakulia donge nono la Dola 3000! Timu ya Watanzania ‘Bongo Starz’ ya jijini Los Angeles iliweza kuichapa Ivory Coast bao 4 kwa 1 bila …
Kliniki ya mafunzo mchezo wa kikapu kuanza Sept 6
Balozi wa Marekani nchini Tanzania kuifungua Na Moshi Stewart, MAELEZO-Dar es Salaam SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini na wadau wengine kama Coca-Cola kupitia kinywaji cha Sprite na Family Healthy International (FHI), wameandaa ziara ya kimichezo ya mafunzo ya ‘Basketball’ yatakayotolewa na wachezaji wa zamani wa ligi kubwa ya mpira wa kikapu …
Pambano la Stars na Algeria laingiza mil 148
PAMBANO la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya timu ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) limeingiza sh.148,220,000. Mechi hiyo ilichezwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,892. Viti vya kijani ambavyo kiingilio …
Guinness yapata wakali wa soka watakaokwenda Afrika Kusini
MASHINDANO ya vipaji vya mpira ya ‘Guinness Football Challenge’ yamemalizika jana katika viwanja vya Leaders na kupatikana timu nane za watu wawili wawili kila timu ambao wanatarajia kupelekwa nchini Afrika Kusini kujiunga katika shule maalumu ya vipaji vya mpira wa miguu. Mashindano hayo ambayo yamezaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) chini ya kinywaji chao cha Guinness yalifanyika jana …
Tevez asema ataheshimu mkataba Man City
CARLOS Tevez amekiri itakuwa “vigumu” kuondoka Manchester City kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili msimu huu. Tevez alikuwa na matumaini angeondoka katika klabu hiyo ili aweze kuwa karibu na mabinti wake nchini Argentina. Lakini taarifa za karibu na mchezaji huyo zimeiambia BBC: “Itakuwa haiwezekani kwa Carlos kuondoka na hilo analifahamu.” Ameongeza kusema klabu ya Inter Milan imemtaka mshambuliaji huyo, …