KIUNGO wa Timu ya Polisi Dodoma, Ibrahim Masawe amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti katika Ligi Kuu ya Vodacom. Masawe alichaguliwa kwenye mechi namba 4 ya ligi hiyo kati ya timu yake ya Polisi Dodoma na African Lyon iliyochezwa Agosti 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu, Masawe alipata alama 93 …
Ujue Msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania inaendelea nchini. Je, wataka kujua timu gani inaongoza na nani anafunga mkia katika msimamo wa ligi hiyo? Basi BOFYA hapa chini ujue msimamo;- MSIMAMO LIGI KUU 2011-12 media
TFF, FIFA waandaa semina kwa wadau wa soka
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) wameandaa semina ya siku tatu itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Oktoba 25-28, 2011 kwenye hoteli ya Peacock. Semina hiyo inalenga kuwaleta pamoja wadau wote muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake. Wadau wakuu ni Serikali, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wadhamini na wanahabari. Lengo …
Vodacom yadhamini mafunzo ya waandishi wa michezo
MAFUNZO kwa ajili ya waandishi wa habari za michezo yatafanyika mkoani Morogoro Oktoba 1 na 2 mwaka huu chini ya udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania. Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando, amesema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuwa maandalizi ya mafunzo hayo …
Kamati ya Nidhamu kukutana Sept 24 kuwajadili Rage, Sendeu
KAMATI ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana tena Septemba 24 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza mashauri matatu dhidi ya Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Louis Sendeu. Awali kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alfred Tibaigana ilikuwa ikutane Agosti 29 mwaka huu …
TFF kuwasilisha mashtaka dhidi ya Sendeu
SEKRETARIETI ya TFF itawasilisha mashtaka dhidi ya Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi inayoongozwa na Kamishna wa Polisi mstaafu Alfred Tibaigana kutokana na matamshi yake dhidi ya mwamuzi Alex Mahagi. Mara baada ya mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyochezwa Septemba 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa …