SHOOTING YAPIGWA FAINI SH. 500,000

KAMATI ya Mashindano ya TFF imeipiga faini ya sh. 500,000 timu ya Ruvu Shooting ya Mkoa wa Pwani baada ya kupata kadi sita kwenye mechi namba 40 ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Septemba 17 mwaka huu Uwanja wa Mlandizi. Akitoa taarifa hiyo jana mjini hapa, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema kwa mujibu wa …

MECHI YA TAIFA STARS NA MOROCCO YAHAMISHWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRMF) limehamisha mechi ya kundi D ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco kutoka Casablanca na sasa itachezwa Marrakech.   Mechi hiyo itachezwa saa 1.30 jioni Oktoba 9 mwaka huu. Pia Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo …

TFF wataka ufafanuzi juu ya mbwa wa polisi

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko tukio la mbwa wa polisi kukata kamba na kusababisha mtafaruku kwa wachezaji wakati wa mechi kati ya Toto Africans na Simba iliyochezwa Septemba 21 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba. Tunafanya mawasiliano na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza ili kujua chanzo cha tukio hilo, na hatua ambazo jeshi hilo …

Taarifa na ufafanuzi masuala anuai kutoka TFF

Kupotea tiketi mechi ya Yanga, Azam Mmoja wa wauzaji tiketi kwenye mechi ya Azam na Yanga iliyochezwa Septemba 18 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Seleman Masoud aliripoti kupotelewa kitabu kimoja cha tiketi mara baada ya ugawaji wa vitabu hivyo kwa wauzaji kufanyika asubuhi ya siku ya mchezo kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). …

Arsenal yalambwa 4-3 na Blackburn

BLACKBURN imepata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya England msimu huu na kumpunguzia ugonjwa wa moyo meneja wao, Steve Kean baada ya kuwa nyuma lakini wakafanikiwa kuilaza Arsenal mabao 4-3 katika uwanja wa Ewood Park. Gunners walikuwa ndio wa kwanza kupata bao lililofungwa na Gervinho kutoka umbali wa yadi 12 lakini Blackburn walisawazisha kwa bao rahisi lililowekwa wavuni …

Stars, Morocco kucheza Oktoba 9

MECHI ya kundi D ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco itachezwa saa 1.30 jioni Oktoba 9 mwaka huu nchini Morocco. Pia Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo pia ziko kundi D zitacheza tarehe hiyo hiyo na muda huo huo ili kuepuka kupanga matokeo. …