Mtihani wa mawakala wa wachezaji wafanyika

MTIHANI wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) umefanyika jana Septemba 29 mwaka huu saa 4 asubuhi kwenye Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisa wa Habari wa TFF, Boniface Wambura, imesema Watanzania wanane walijisajili kwa ajili ya kufanya mtihani huo. Watano …

Azam FC wawalalamikia waamuzi VPL

TIMU ya Soka ya Azam FC imelalamikia vitendo vya baadhi ya waamuzi wa Soka ndani ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, kwa kile kutoa upendeleo kwa baadhi ya timu. Kwa mujibu wa taarifa na mkanda wa video ambao Azam FC imeutoa kwenye mtandao wake, imeoneshwa kutoridhishwa na mwenendo wa waamuzi kwani wamekuwa wakikandamiza baadhi ya vilabu. “Inawezekana Ngasa alikuwa offside …

Poulsen aita 23 kuikabili Morocco

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen Septemba 27 mwaka huu ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Morocco. Akitoa taarifa hiyo jana mjini Dar es Salaam Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema kikosi hicho kitaingia kambini Septemba 29 …

Mechi ya Simba, Mtibwa zaingiza mil. 74

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa Septemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 74,345,000. Akizungumza na wanahabari leo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura amesema watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 13,285 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, …

Wenger: Kuvurunda kumeiathiri Arsenal kiuchumi

ARSENE Wenger amekiri kiwango cha chini cha soka kwa timu yake ya Arsenal kilichangia kupungua kwa mashabiki wake uwanjani wakati timu hiyo ilipocheza na Bolton siku ya Jumamosi. Lakini meneja huyo wa Arsenal ameonya kwamba mdororo wa uchumi unaoelekea kuikumba dunia huenda ukasababisha pia mashabiki kupungua katika viwanja mbalimbali vya soka England. “Kwanza tulikuwa na matokeo mabaya hivi karibuni na …