Marrakech, Morocco TAIFA Stars imewasili salama hapa Marrakech, Morocco tayari kwa mechi dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Oktoba 9 mwaka huu saa 1.30 usiku kwa saa za hapa. Kuna tofauti ya saa 3 kati ya hapa na Tanzania, hivyo kwa saa za nyumbani mechi itakuwa saa 4.30 usiku. Timu ilitua Casablanca saa 9.30 ikitokea Doha, Qatar ambapo ililala juzi Alhamisi …
Timu ya 94KJ yaanza vema mechi za majaribio
Na Mwandishi Wetu ZIKIWA zimesalia siku nne kabla ya ratiba ya Ligi Kuu Daraja la Kwanza kuanza timu ya soka ya 94KJ yenye maskani yake Uwanja wa Vinyago Mwenge jijini Dar es Salaam inaendelea na maandalizi yake kwa kucheza mechi za kirafiki, ambapo tayari wiki hii imecheza mechi za kujipima nguvu. Siku ya Jumanne timu hiyo ilishuka dimbani katika Uwanja …
Taifa Stars kuagwa Oktoba 6
TAIFA Stars inatarajiwa kuagwa Oktoba 6 mwaka huu saa 4 asubuhi kambini kwao hoteli ya Chichi iliyoko Kinondoni, Dar es Salaam kabla ya kuondoka siku hiyo hiyo mchana kwenda Casablanca kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco. Mechi hiyo ya mwisho ya mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani katika nchi za Equatorial Guinea …
Nsajigwa aumia mazoezini, wachezaji wa kulipwa waanza kuwasili
Na Mwandishi Wetu NAHODHA wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa ameumia nyonga (groin) kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo Oktoba 3 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa daktari wa Taifa Stars, Dk. Mwanandi Mwankemwa, maumivu hayo yatamweka Nsajigwa ambaye pia ni Nahodha wa Yanga nje ya uwanja kwa kati ya wiki mbili hadi nne. …
RC Morogoro awaasa waandishi wa michezo
Na Mwandishi Wetu, Morogoro MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera amewataka waandishi wa habari za michezo kuacha dhana potofu ya kuripoti habari za uchochezi na badala yake waripoti habari zinazoelimisha jamii kwa ujumla. Bendera ametoa kauli hiyo leo wakati wa semina ya waandishi wa habari za michezo waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini …
TFF yazionywa klabu Ligi Kuu ni kuhusu ada
WAKATI Ligi Daraja la Kwanza imepangwa kuanza Oktoba 15 mwaka huu, klabu saba kati ya 18 bado hazijalipa ada ili timu zao ziweze kushiriki katika ligi hiyo iliyogawanywa katika makundi matatu. Klabu ambazo hazijalipa ada ya kushiriki ya sh. 200,000 ni AFC ya Arusha, Majimaji ya Ruvuma, Polisi ya Iringa, Polisi ya Tabora, Rhino Rangers ya Tabora, Small Kids ya …