Michuano Ligi Daraja la Kwanza na ratiba
MICHUANO ya Ligi Daraja la Kwanza hatua ya makundi msimu huu inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaanza Oktoba 15 mwaka huu. Jumla ya timu 18 zinashiriki katika ligi hiyo. Kundi A kesho itakuwa Temeke United vs Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa Mlandizi, Pwani) na Mgambo Shooting vs Transit Camp (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga). Mechi nyingine ya kundi …
Mtanzania aombewa ICT Ujerumani, Viingilio Simba Vs Lyon vyatajwa
MCHEZAJI Costancia Maringa wa Tanzania ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili aweze kucheza mpira wa miguu wa wanawake nchini Ujerumani. Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB) kimetuma maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya FC 1919 Marnheim ya nchini humo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa DFB, Helmut …
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TASWA Desemba 17, 2011
KAMATI ya Utendaji ya TASWA iliyokutana hivi karibuni, ilifikia uamuzi wa mkutano huo ufanyike eneo hilo lililopo Kilometa 37 kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kuwaweka pamoja kwa siku nzima waandishi wa habari za michezo na kubadilishana mawazo kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyotokea mwaka 2011. Nia ya TASWA ni kumaliza Mkutano Mkuu saa nane mchana …
Tanzania yafungwa 3-1 na Morocco
Marrakech, TANZANIA (Taifa Stars) imefungwa mabao 3-1 na Morocco katika mechi ya mchujo kuwania tiketi ya AFCON 2012 iliyochezwa leo hapa Grand Stadium na kushuhudia na maelfu ya watazamaji kwenye uwanja huo wenye viti 43,000. Hadi mapumziko matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1. Wenyeji Morocco ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 19 mfungaji akiwa Marouane Chamakh kwa mpira wa kichwa …
Jan Poulsen ataja kikosi cha kwanza
KOCHA Jan Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 11 ambao wataanza kwenye mechi ya leo dhidi ya Morocco. Mechi hiyo inaanza saa 1.30 usiku kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania ni saa 4.30 usiku na itachezwa Grand Stadium hapa Marrakech. Poulsen atatumia mfumo wa 4-4-1-1 huku akimweka Mbwana Samata kuwa mshambuliaji wa mwisho na nyuma yake akicheza Abdi Kassim. Katika …