Wenger hana hofu mkataba wa Van Persie

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hana wasiwasi kwamba Robin van Persie si mwenye haraka ya kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo. Nahodha wa Arsenal, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2013, amesisitiza “nafsi yake imejitolea kwa klabu ya Arsenal”. Wenger amesema: “Iwapo utakuwa umejiwekea asilimia 100 hadi siku ya mwisho ya mkataba wako, hiyo yote naiita ni kujifunga kabisa. “Kwangu …

WEST BROM YAITUNISHIA MISULI WOLVES KWA 2-0

Katika ligi ya Ungereza West Bromwich Albion katika mchezo ulioanza mapema imefanikiwa kuzoa pointi tatu baada ya kuilaza Wolves mabao 2-0 na kufanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa nyumbani na kujikwamu eneo la kushuka daraja. Chris Brunt alikuwa wa kwanza kuipatia West Brom bao la kuongoza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Billy Jones. Kevin Doyle naye alikaribia kuipatia bao …

Arsenal yaikomalia Sunderland kwa 2-1.

Mabao mawili mazuri aliyofunga Robin van Persie yameiwezesha Arsenal kupata ushindi dhidi ya Sunderland katika uwanja wa Emirates. Nahodha huyo wa Arsenal alifunga bao la kwanza katika sekunde ya 29 tangu mchezo ulipoanza, bao linaloonekana ni la mapema sana kufungwa katika Ligi Kuu ya England msimu huu. Lakini ilionekana kama Sunderland ingepata pointi katika mchezo huo baada ya mchezaji wa …

Man United yang’ang’aniza sare na Liverpool

Javier Hernandez aliisawazishia Manchester United zikiwa zimesalia dakika tisa kabla mchezo haujamalizika na kuisaidia timu yake kuambulia angalao pointi moja katika pambano kali dhidi ya Liverpool. Mshambuliaji huyo anayechezea pia timu ya taifa ya Mexico, aliingizwa mchezaji wa akiba kipindi cha pili, alitumia akili ya haraka baada ya mpira uliochongwa na Danny Welbeck na kufanikiwa kuisawazishia kwa kichwa timu yake …

Aston Villa yaipeleka Man City Kileleni

Manchester City imetumia mwanya wa Man United kuteleza kwa kwenda kileleni baada ya kuizaba Aston Villa 4-1. Kipa wa Man City, Joe Hart aliokoa mkwaju wa Gabriel Agbonlahor mapema, kabla ya Mario Balotelli kufunga goli maridadi la kwanza. Adam Johnson aliandika bao la pili baada ya Stephen warnok kufanya makosa, huku Vincent Kompany akiandika bao la tatu baada ya kuunganisha …