Hofu imeanza kutanda kwa mashabiki wa soka nchini humo jambo hili linaweza kuwatoa Uingereza katika michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Russia ,Endapo bunge litapiga kura wiki ijayo basi itaiweka Uingereza katika hali ya sintofahamu juu ya ushiriki wao katika kombe la dunia la mwaka 2018. Mgogoro kati ya bunge la Uingereza na FA unakuja baada ya baadhi ya …
Timu ya Wanahabari Iringa Yapigwa Tafu na Mbunge
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akimkabidhi mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoani Iringa moja ya jezi alizotoa kwa waandishi wa habari kwa ajili ya mechi mbalimbali za timu hiyo. Na Fredy Mgunda, Iringa MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari mkoa wa Iringa kwa kuwapatia jezi seti …
Chuo cha CBE Waibuka Vinara ‘TTCL Inter College Beach Soccer’
Na Mwandishi Wetu CHUO cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE) kimeibuka vinara wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni ‘TTCL Inter College Beach Soccer’ yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kupitia kocha wa taifa wa mpira huo wa ufukweni nchini. Chuo cha …
Meneja wa Crystal Palace Atimuliwa
Klabu ya Crystal Palace imemfuta kazi mkufunzi wake Alan Pardew wakati ambapo klabu hiyo iko katika nafasi ya 17 katika ligi ya Uingereza. Pardew aliteuliwa na kupewa kandarasi ya miaka mitatu na nusu katika mkataba uliotiwa sahihi mnamo mwezi Januari 2015, lakini meneja huyo mwenye umri wa miaka 55 amefutwa kazi baada ya kushinda mechi moja pekee kati ya 11. …
Tanzania Viwango vya FIFA Bado Tia Maji
Taifa la Guinea-Bissau ndio taifa lililofaidika sana katika orodha mpya ya shirikisho la soka duniani Fifa mwaka 2016 baada ya kupanda nafasi 78 tangu Disemba mwaka uliopita. Taifa hilo sasa limeorodheshwa la 68 katika orodha ya dunia na la 15 barani Afrika. Hatua hiyo inamaanisha kwamba Guinea Bissau ipo juu ya mataifa ya Uganda ,Togo na Zimbabwe ambayo pia yamefuzu …
Leicester City Yatwaa Tuzo ya Klabu Bora
Klabu ya soka ya Leicester imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka kwa kuwashangaza wengi waliposhinda ligi ya Uingereza. The Foxes kama inavyojiita ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka na mkufunzi wake Claudio Ranieri alitangazwa kuwa kocha bora baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji hilo. Leicester ilianza kampeni ya kushinda taji hilo bila wengi kutarajia baada ya kushushwa …