Mmarekani Ginny Thrasher amekuwa mwanamichezo wa kwanza kushinda dhahabu katika Michezo ya Olimpiki Rio baada ya kutwaa ushindi katika shindano la kulenga shahaba kwa bunduki kutoka mita 10 upande wa wanawake. Huo ndio ushindi wa kwanza katika shindano kubwa la kimataifa kwa mwanamichezo huyo wa umri wa miaka 19. Thrasher alipata alama 208.0 huku bingwa wa dunia mwaka 2006, Mchina …
Azam Fc Wavuta Vifaa Vipya Kuimalisha Ulinzi
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, leo jioni imeingia mkataba na mabeki wawili, Mghana Daniel Amoah na Mzimbabwe, Bruce Kangwa, kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao. Wawili hao kila mmoja amesaini mkataba wa miaka mitatu, Amoah anayecheza beki ya kati ametokea Medeama ya Ghana, huku Kangwa aliyefuzu majaribio ya kujiunga na Azam FC akitokea kwa …
Sherehe za Michuano ya Olimpiki Ndani ya Jiji la Rio Brazil
5.50am:Na mwenge wa Olympic uliowasili katika uwanja wa Mariccana unapokezwa aliyekuwa mwanariadha wa mbio za Marathon nchini Brazil Vanderlei Cordeiro de Lima – Ambaye anauwasha mwanga katika uwanja huo ishara ya ufunguzi rasmi ya michezo hiyo 5.32am:Wimbo wa taifa la Brazil unaimbwa kwa sasa katika ukumbi wa ufunguzi wa michezo hiyo 5.20am:Uwanja wa Mariccana ulivyofurika maelefu ya mashabiki 5.15am:Bendera zote …
Jeuri ya Fedha Yaanza Kutema cheche Msimbazi wavuta Mshambuliaji
SIKU chachea baada ya mfanyabiashara maarufu nchini na mwanachama wa Simba SC, Mohammed Dewji ‘Mo’ kuichangia klabu hiyo shilingi milioni 100 za usajili, hatimaye wamefanikiwa kumleta mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo. Mavugo ambaye ametokea nchini Ufaransa alikokwama kujiunga na klabu ya Tours ya Ligi Daraja la Pili, maarufu kama Ligue 2 ametua usiku wa Jumatano August 3 jijini …
Ahmed Musa wa Leicester City Apiga Mbili mwenyewe Mbele ya Barcelona
Mchezaji ghali zaidi kununuliwa na Leicester City Ahmed Musa, aliyenunuliwa pauni milioni 16 na kuvunja rekodi ya klabu hiyo, amewafungia mabao yote mawili katika mechi ambayo wamefungwa 4-2 na Barcelona katika michuano ya Kombe la Kimataifa la Klabu. Munir alifungua ukurasa wa mabao kupitia pasi iliyotoka kwa Lionel Messi kabla ya nyota huyo wa Argentina muda mfupi baadaye kumuandalia pasi …
Masaa Machache Yasalia Kabla Pazi la Olimpiki Kufunguka
Mashindano ya Olimpiki mjini Rio kufunguliwa rasmi kesho Ijumaa, lakini hali bado haijakaa vizuri katika mazingira ya michezo hiyo. Vilabu mbali mbali barani Ulaya vinajiweka tayari kwa msimu ujao yamebakia masaa tu hadi kuanza rasmi michezo ya 31 ya Olimpiki mjini Rio. Mahakama ya kimataifa ya michezo inachukua hatua za haraka kuamua rufaa zilizopelekwa katika mahakama hiyo na wanariadha wa …