Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena leo kwa michezo miwili ambapo katika mchezo wa kwaza Manchester United waliisambaratisha Klabu ya AFC Bournemouth kwa mabao 3 – 1 yakifungwa na Mata, Zlatan pamoja na Rooney wakati lile la AFC Bournemouth likifungwa na Adam Smith Nayo Arsenal wakiwa nyumbani kwao waliangukiwa na kichapo cha mabao 4 kwa 3 dhidi ya Liverpool,Mabao ya …
Kama Riadha Basi Mfalme ni Mo Farah
Mo Farah amekuwa mwanariadha wa kwanza wa Uingereza wa mbio na uwanjani kushinda nishani tatu za dhahabu katika michezo ya olimpiki, baada ya kuwaonyesha wakenya na waethiopia kivumbi, na kushinda mbio za mita 10,000 mjini Rio. Mwanariadha huyo, aliye na umri wa miaka 33, alijikwaa wakati wa mbio hizo, japo alijikakamua vilivyo katika mita 100 za mwisho na kushinda kwa …
Klabu ya Yanga Yalimwa Faini na TFF
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), leo saa 6:00 usiku litafunga tena dirisha la usajili baada ya kulifungua jana kwa saa 48 na imebainika kuwa timu tatu zaidi zilikuwa na dosari katika usajili hivyo kufanya ongezeko la kutoka timu nane zilionekana kwa haraka mapema wiki hii mara baada ya dirisha kufungwa Agosti 6, 2016. Timu hizo kwa ujumla …
Simba na URA Watoana Jasho Uwanja wa Taifa
Wekundu wa Msimbazi Simba leo wamelazimishwa sare goli 1-1 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda uliochezwa kwenye uwanja wa taifa URA walianza kupata bao lililofungwa na Nkugwa Elkanah 19kipindi cha kwanza lakini Jonas Mkude alisawazisha bao hilo dakika ya 31 kwa kuunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na beki wa kushoto Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr. …
Leicester City Waanza Ligi Kuu Uingereza Kwa Kichapo
Mabingwa watetezi wa Ligi ya England Leicester City wameanza msimu wa 2016/17 kwa kuchapwa ugenini na Hull City. Leicester wamechapwa 2-1, mabao ya Hull yakifungwa na Adama Diomande (46+2′) na Robert Snodgrass (55′). Bao la kufutia machozi ya Leicester City limefungwa na Riyad Mahrez kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 47. Leicester City ndio mabingwa wa kwanza watetezi kushindwa mechi …
Yanga Yaleta Matumaini kwa Kuifumua Mo Bejaia Taifa
YANGA SC imefufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kufuatia ushindi wa 1-0 jioni ya leo dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria katika mchezo wa marudiano Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Shukrani kwake, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Josleyn Tambwe aliyefunga bao hilo pekee mapema tu kipindi cha kwanza. Ushindi huo …