Barcelona Yaanza Vyema Ligi ya Mabingwa Ulaya

Celtic walipokezwa kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou. Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga ‘hat-trick’ yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C.Alianza kwa kufunga bao la mapema. Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili. Kipindi cha pili, …

Semina Kubwa ya Mchezo wa Karate Yaanza Jijini Dar

Anafundisha kwa mifano! Shihan Okuma akishambuliwa na Jerome Sensei kama sehemu ya maelekezo katika semina hiyo Na Daniel Mbega SEMINA kubwa ya Shotokan Karate kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, imeanza leo hii jijini Dar es Salaam ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo nchini Tanzania, inaongozwa na mkufunzi mkuu, Shihan Koichiro Okuma (6th Dan), kutoka makao makuu …

Timu za Taswa SC Zatamba Bonanza la Waandishi wa Habari Arusha

  Nahodha wa timu ya Netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC)Zuhura Abdulnoor na mchezaji mkongwe wa Timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini,(Taswa FC),Muhidin Sufiani(kulia)wakifurahia ushindi.   Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akizungumza katika Bonanza la 11 la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha. Mchezaji nguli wa timu ya …

Kaseja Akumbukwa Soka la Ufukweni

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Ufukweni, John Mwansasu amemuita Kipa wa Mbeya City ya Mbeya, Juma Kaseja Juma kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kinachotajia kusafiri kwenda Abidjan kucheza na wapinzani wao Ivory Coast kwenye mchezo wa marudiano wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. Kaseja mwenyewe, amefurahia wito …

Ratiba ya Ligi Daraja la Pili Sasa Hadharani

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa orodha ya makundi manne na timu zitakazoshiriki Ligi Daraja la Poli ((SDL) inayotarajiwa kuanza baadaye, mwaka huu. Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi (TPLB), chombo maalumu cha kusimamia michezon inayoendeshwa na TFF makundi na timu hizo ni kama ifuatavyo. Kundi A Bulyanhulu FC- Shinyanga Geita Gold SC- Geita Mashujaa FC- Kigoma Milambo …

Simba na Azam Kukutana Septemba 21

Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Azam FC na Simba ya Dar es Salaam, utafanyika Jumatano Septemba 21, 2016 badala ya Septemba 17, mwaka huu. Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, umesogezwa mbele kuipisha timu ya taifa ya Congo-Brazzaville ipate nafasi ya kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, ikiwa ni kutekeleza matakwa …