Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi kuendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za kuleta mabadiliko nchini Burma. Katika ziara yake fupi ya kihistoria, Obama alikutana na Rais Thein Sein na kusema uamuzi wa mwisho kuhusu kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Burma kutategemea jinsi taifa hilo litakavyoshughulikia malalamishi yaliyokuwa yametolewa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu. Aidha Obama alikutana na mwanaharakati …
Majeshi ya Israel Yaendelea Kushambulia Gaza, Makao Makuu Hamas Yapigwa
ISRAEL imeshambulia maeneo ya wapiganaji katika ukanda wa Gaza kwa siku ya tano (Novemba 18, 2012), wakishambulia kwa ndege na jeshi la majini wakati jeshi lake lingine likijitayarisha kufanya mashambulizi ya ardhini. Misri hata hivyo inaona ishara za uwezekano wa kupatikana usitishaji wa mapigano hapo katika siku za baadaye. Wapalestina 47, karibu nusu yao wakiwa ni raia, ikiwa ni pamoja …
Kamanda wa Boko Haram Auawa Nigeria
WANAJESHI wa Nigeria wanaendeleza operesheni kali ya kuwasaka wapiganaji wa Boko Haram katika eneo la Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Wanajeshi hao wanatumia magari ya kivita na wanapewa usaidizi zaidi na helikopta za kijeshi. Jeshi la Nigeria limedai kuwa limemuua kamanda mmoja mwandamizi wa Boko Haram Ibn Saleh Ibrahim. Raia wa eneo hilo wamesema kuwa idadi kubwa ya watu …
Waziri Mkuu wa Misri Aitembelea Gaza, Wapalestin Waomba UN Iingilie
WAZIRI Mkuu wa Misri Hisham Kandil ameutembelea Ukanda wa Gaza na kuahidi kuwasaidia Wapalestina kurejesha utulivu kwa kusitisha mashambulizi ya Israel ambayo yameendelea licha ya ziara hiyo. Wakati huo huo Wapalestina nao wamerudia wito wao kwa Umoja wa Mataifa wakiutaka kuingilia kati mashambulizi yanayofanywa na Israel katika ukanda huo. Waziri Mkuu huyo wa Misri amewaahidi Wapalestina kuwa nchi yake itafanya …
Mapigano Mapya Yazuka Congo
MAPIGANO mapya yamezuka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kati ya wanajeshi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na waasi wa M23,na kuwalazimisha watu kukimbia makaazi yao. Tarifa kutoka eneo la tukio zinasema kumekuwa na mapigano makali ya silaha kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo la Kivu kaskazini, Goma. Watu wapato 50,000 hawana mahali pa kuishi tangu mwezi Aprili …
Israel Yasema Itajilinda Kivyovyote Dhidi ya Mashambulizi ya Gaza
WAKATI mzozo kati ya Hamas na Israel ukizidi kufukuta ukanda wa Gaza, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema nchi yake itachukua kila hatua za kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Gaza. Netanyahu ameyasema hayo leo jioni alipozungumza na waandishi wa habari akizungumzia vitendo vya wanamgambo wa Kipalestina kutoka Gaza. “Kwa saa 24 zilizopita Israel imeweka sawa kabisa kwamba haitavumilia …