MKUU WA MAJESHI nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo. Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia Mutomboki. Msemaji wa …
Jaribio la mapinduzi yatibuliwa Sudan
Watu kadhaa wamekamatwa na serikali ya Sudan, wakiwemo mkurugenzi mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi, Salah Gosh na maafisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo kufuatia madai ya kujaribu kupindua serikali ya nchi hiyo. Raia kadha wamesema wameona magari kadhaa ya kivita na wanajeshi wakishika doria katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum. Katika miezi ya hivi …
Mke wa Gbagbo kufikishwa the Haque
MAHAKAMA ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi Simone, Gbagbo. Bi Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya uchaguzi wa urais nchini humo. Mumewe tayari amekamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo …
JK Atuma Rambirambi kwa Rajani Group of Companies
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameitumia salamu za rambirambi familia ya Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni la Rajani Group of Companies, Mzee Jayantilal Pragji Rajani kufuatia kifo cha mzee huyo kilichotokea Novemba 21, 2012, mjini London, Uingereza. Katika salamu zake kwa familia hiyo, Rais Kikwete ameeleza masikitiko na huzuni yake kufuatia taarifa za kifo cha …
Kanisa la Anglikana Lateuwa Askofu wa Kwanza wa Kike
ELLINAH Wamukoya ameteuliwa kuwa Askofu wa Kwanza wa Kike wa Kanisa la Kianglikana barani Afrika. Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo ni heshima kwa kina mama. Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa kanisa hilo katika ufakme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata siasa za kihafidina. Kutawazwa kwake kumejiri huku …
Waasi wa M23 Wauteka Mji wa Goma
WAPIGANAJI wa waasi wa M23, hatimaye wamefanikiwa kuingia mji mkuu wa eneo la Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini. Mwandishi wa BBC mjini Goma anasema wapiganaji hao wa waasi walikabiliana kwa risasi na wanajeshi wa serikali, ambao walitoroka baada ya kuzidiwa nguvu. Jeshi la Umoja wa Matifa la Kutunza amani katika eneo hilo …