Wapinzani Wapinga Kujadiliana na Mursi, Ikulu Yavamiwa

RAIS Mohamed Mursi leo Desemba 08, 2012 alitarajiwa kufanya mazungumzo juu ya kumaliza mzozo mbaya nchini Misri tangu achukue madaraka. Hata hivyo viongozi wakuu wa upinzani nchini humo wameapa kuwa hawatashiriki mazungumzo hayo. Cairo pamoja na miji mingine imekumbwa na maandamano ya vurugu tangu Novemba 22, wakati Mursi alipotangaza amri akijipa madaraka makubwa zaidi ambayo yanamuweka juu ya sheria. Mvutano …

Jeshi Lawatimua Waandamanaji Misri

WANAJESHI nchini Misri wameanza kuwaondoa watu kutoka katika eneo la Ikulu ya rais mjini Cairo ambako kumekuwa na makabiliano makali kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi. Limetuma vifaru na magari mengine yaliyo hamiwa kwa silaha nje ya kasri la rais baada ya mapigano ya usiku kucha kati ya wafuasi na wapinzani wa Rais Mohammed Morsi. Walioshuhudia matukio …

Rushwa Yazorotesha Uchumi Duniani

RIPOTI ya mwaka huu ya Shirika la Kimataifa linalopambana na ufisadi duniani (Transparency Intenational) inaeleza kuwa rushwa imechochea kwa kiasi fulani mgogoro wa uchumi duniani, huku Somalia na Korea Kaskazini zikiongoza. Pamoja na kuwepo kwa kampeni mbalimbali na katika maeneo tofauti duniani dhidi ya ufisadi, lakini faharasa ya rushwa ya shirika la Transparency International inaonesha kuwa theluthi mbili kati ya …

Urais Kenya: Raila Aungana na Kalonzo

WAZIRI Mkuu wa Kenya, Raila Odinga kupitia chama chake cha ODM wametia saini makubaliano ya kuunda muungano wa kisiasa na Makamo wa Rais Kalonzo Musyoka ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa taifa hilo utakaofanyika mwezi Machi 2013. Huu utakuwa muungano wa pili kabla ya tarehe ya mwisho (04-12-2012) iliyowekwa na msajiri wa vyama vya siasa iliyotaka vyama hivyo viwe …

Rwanda Iliwasaidia Wafuasi wa M23 Kuuteka Mji wa Goma- UN

RIPOTI ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyotolewa inasema wanajeshi kutoka Rwanda walihusika moja kwa moja na utekaji wa Mji wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliotekelezwa na waasi. Ripoti hiyo iliyokusanywa kwa ajili ya Baraza la Usalama, inasema wanajeshi 500 wa Rwanda, walihusika katika utekaji huo wa kundi la M23. Msemaji mmoja wa Jeshi la Rwanda amesema kuwa …

Uingereza Yasitisha Msaada kwa Rwanda

Uingereza imesitisha kwa muda msaada iliyokuwa iipe Rwanda kwa sababu ya wasiwasi kuhusu kuhusika kwa nchi hiyo katika mzozo uliopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mawaziri walisema kwamba Uingereza sasa haitatoa msaada wa pauni milioni 21. Rwanda ilipewa msaada wa kiasi cha pauni milioni 16 mnamo mwezi Septemba, hata baada ya tashwishi kuwepo kuhusu tetesi kwamba ilikuwa inawaunga mkono wanamgambo …