RAIS wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, anayetibiwa kwa ugonjwa wa mapafu, anaendelea vyema na matibabu yake na kwamba hali yake imeimarika katika saa 24 zilizokamilika. Taarifa za kuugua kwa Mandelea zimewatia watu wasiwasi mkubwa hasa wapenzi wa mpiganiaji haki huyo. Bwana Mandela,mwenye umri wa miaka 94, alikimbizwa katika hospitali ya kijeshi, mjini Pretoria, siku ya Jumamosi. Madaktari …
Kenya Waadhimisha Miaka 49 ya Uhuru
SIKU ya Jamhuri ni maadhimisho ya siku Kenya ilipotangazwa kuwa huru baada ya kutawaliwa na wakoloni waingereza waliokuwa wakiwakandamiza waafrika weusi katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Leo ni siku ya uhuru wa Kenya, ambapo Wakenya wanaadhimisha miaka 49 ya Siku ya Jamhuri katika sherehe maalum zinazofanyika katika uwanja wa kitaifa wa michezo wa Nyayo. Rais Mwai Kibaki anawaongoza Wakenya …
Waziri Mkuu wa Mali Ajiuzulu
WAZIRI Mkuu wa Mali, Cheick Modibo Diarra amejiuzulu wadhifa wake saa chache baada ya kukamatwa na wanajeshi waliomkuta nyumbani kwake. Kujiuzulu huko kunaupeleka pabaya zaidi mzozo unaoendelea kuikumba nchi hiyo. Tangazo la Cheick Modibo Diarra kujiuzulu wadhifa wake ambalo limerushwa na kituo cha taifa cha utangazaji, lilikuwa fupi. “Mimi Cheick Modibo Diarra najiuzulu pamoja na serikali yangu,” alisema katika tangazo …
Hali ya Taharuki Yatanda Misri
HALI ya usalama imeimarishwa nchini kote Misri huku Cairo ikijiandaa kwa maandamano mengine yanayowahusisha wafuasi na wapinzani wa katiba mpya iliyopitishwa na serikali ya Misri. Wanajeshi wanafanya doria kwa kutumia vifaru huku wakiwa wameweka vizuizi vya seng’enge na matofali, nje ya Ikulu ya Rais Mohammed Morsi. Makundi ya upinzani yanataka kura ya maoni ifutwe iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi juu …
Jeshi la Sudan Kusini Lauwa Watu 10, Waasi M23 Wazungumza na Serikali
UMOJA wa Mataifa unasema kuwa Jeshi la Sudan Kusini limewapiga risasi na kuwauwa watu 10, ambao walikuwa wakiandamana kupinga kuhamishwa kwa Makao Makuu ya Serikali za mitaa magharibi mwa nchi. Ofisa wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa huko Bahr el-Ghazal amesema watu wane waliuwawa katika mji wa Wau kwenye mapambano ya jana usiku. Na wengine sita waliuwawa baada ya …
Rais Mursi Aitisha Mjadala wa Kitaifa
RAIS Mohammad Mursi wa Misri amewaalika wapinzani nchini humo kufanya mazunguzo kwa lengo la kumaliza mgogoro unaoendelea nchini humo. Lakini maandamano dhidi yake na chama chake cha Udugu wa Kiislamu bado yanaendelea. Akihutubia taifa baada ya siku kadhaa za vurugu, Mohammad Mursi aliitisha mkutano wa mjadala wa kitaifa jana. Lakini hakutakuwa na kucheleweshwa kwa kura ya maoni juu ya katiba …