MAELFU ya watu wamekusanyika katika mji wa Bethlehem kwenye Mamlaka ya Wapalestina kusheherekea sikukuu hiyo. Mji huo unaaminika kuwa ndiko pahala alikozaliwa masiha bwana yesu kristo. Misa kubwa ilifanyika usiku wa kuamkia kwenye kanisa kongwe mjini humo na kuhudhuriwa na Rais Mahmoud Abbas. Padri Mkuu wa kanisa Katoliki kwenye eneo la Mashariki ya Kati, Fuad Twal ndiye aliyeongoza misa hiyo …
Mandela Kusalia Hospitalini Krismasi
Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela atasalia hospitalini msimu huu wa Krismasi. Bwana Mandela ambaye ni rais mweusi wa kwanza nchini Afrika Kusini, alilazwa hospitali wiki mbili zilizopita kufuatia maambukizi ya mapafu na uvimbe au mawe kwenye kibofu. Kuna wasi wasi mkubwa nchini Afrika kuhusu afya yab rais huyo wa zamani mwenye umri …
Makaburi zaidi yavunjwa Timbuktu
Taarifa kutoka kaskazini mwa Mali zinaeleza kuwa wapiganaji wa Kiislamu wamevunja makaburi kadha ya kale katika mji wa Timbuktu. Wapiganaji wax Kiislamu nje ya Timbuktu Kiongozi mmoja wa wapiganaji hao ameliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba makaburi yote mjini Timbuktu yatavunjwa, kwa sababu yanakwenda kinyume na Uislamu. Kati ya mwaka huu makaburi kadha yalivunjwa katika mji huo ambao ni …
Wapiganaji wa CAR wasonga mbele
Wapiganaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameuteka mji wa Bambari, mji wa tatu kwa ukubwa. Huo ni mji wa sita kutekwa na wapiganaji hao tangu kuanza kupigana awali mwezi huu, na ndio karibu kabisa na mji mkuu, Bangui, kwa wapiganaji hao kuwahi kufika. Msemaji wa shirika la msaada wa matibabu, Medecins Sans Frontieres, ameeleza kuwa watu wengi wamekimbia makwao …
Baragoi Kenya wavamiwa na kuporwa mifugo
HABARI kutoka Kenya zinasema watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wamevamia kijiji kimoja karibu na mji wa Baragoi, kaskazini magharibi mwa Kenya na kuiba mamia ya mifugo. Majambazi hao karibu mia mbili wanasemekena kuwa na silaha nzito. Watu wengi wameripotiwa kuhama eneo hilo. Zaidi ya polisi arobaini waliuawa na wezi wa mifugo katika eneo hilo la Baragoi mwezi Novemba mwaka huu. Bunge …
Ndege ya UN yashambuliwa Sudan Kusini
UMOJA wa Mataifa umesema helicopta kutoka kwa kikosi chake cha kutunza amani Sudan Kusini imeangusha na jeshi la nchi hiyo na kuwaua watu wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema ndege hiyo ilishambulia wakati ilipokuwa katika harakati za kushika doria Mashariki mwa jimbo la Jonglei. Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduado del Buey amesema …