MARAIS wa Sudan na Sudan Kusini wamekubaliana Januari 5, 2013 kuhusu muda utakaopangwa kwa ajili ya utekelezaji wa masuala muhimu, wakati walipokutana kwa faragha katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Usalama, mafuta na mipaka ni miongoni mwa masuala ambayo rais wa Sudan ya kusini Salva Kiir na mwenzake wa Sudan Omar Hassan al – Bashir waliyajadili mjini Addis Ababa …
NPP Mahakamani Kupinga Matokeo Ghana
CHAMA Kuu cha Upinzani nchini Ghana kimewasilisha kesi katika mahakama kuu zaidi nchini humo kupinga ushindi wa rais John Mahama katika uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi huu. Chama cha National Patriotic Party (NPP) kimepinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika tarehe Saba Desemba, ikidai ulikumba na udanganyifu mkubwa. Tume ya uchaguzi nchini humo ilisema kuwa Bwana Mahakama alipata asilimia 50.7 …
Marekani Yaondoa Wafanyakazi wake Bangui
SERIKALI ya Marekani, imesema imewaondoa raia wake katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kuingia mji mkuu wa nchi hiyo Bangui. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema haijavunja uhusiano wake wa kibalozi na serikali ya nchi hiyo, ila imechukua tahadhari kuhusu usalama wa raia wake. Marekani pia imeonya raia wake dhidi ya kwenda nchini …
Jamhuri ya Afrika ya Kati yaomba msaada wa Ufaransa
SERIKALI ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imevitaka vikosi vya kulinda amani vya Ufaransa kusaidia kusimamisha juhudi za waasi kuendelea kusonga mbele katika harakati zao za kuingia katika mji mkuu Bangui. Mamia ya watu wamekusanyika jana nje ya ubalozi wa Ufaransa wakiwasilisha ombi hilo, ambalo Ufaransa haijajibu haraka lakini imesema wanajeshi zaidi wa kulinda amani wametumwa kuweka ulinzi katika ubalozi …
Hatimaye Nelson Mandela Aruhusiwa kurudi nyumbani
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela, ameruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali moja mjini Pretoria. Ikulu ya rais nchini humo imesema rais huyo wa zamani wa Afrika kusini, anaendelea kupata nafuu nyumbani mwake. Msemaji wa serikali amesema Mandela bado hajapoa kabisa na ataendelea kupokea matibabu nyumbani mwake mjini Johannesburg. Mandela alilazwa hospitaini siku kumi na nane zilizopita kufuatia maambukizi ya …
Mlipuko mkubwa umetokea mjini Lagos
Maafisa wa kuzima moto wakiendelea na kuzima moto katika ghala moja lililolipuka LagosMoto mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Nigeria Lagos.Taarifa zinaarifu kuwa moto huo ulianza katika eneo la kuhifadhi baruti na kisha kuenea kwa haraka katika majengo mengine yaliyo karibu na ghala hilo. Moshi mkubwa umeenea kote katika kisiwa cha Lagos na wazima moto wanajithidi kuuzima moto huo.Bado baadhi …