JIMBO moja nchini Nigeria limetangaza hali ya hatari kutokana na uhaba mkubwa wa nyanya. Jimbo hilo la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria, limechukua hatua hiyo baada ya wadudu waharibifu wajulikanao kama Tomato Leaf Miner au Tuta Absoluta kuharibu nyanya mashambani. Kamishna wa Kilimo katika jimbo hilo Daniel Manzo Maigar amesema wadudu hao wameharibu 80% ya nyanya katika jimbo hilo. Amesema wakulima …
Clinton: Siwezi Kushindwa na Bernie Sanders
Mgombea urais anayeongoza katika chama cha Democratic nchini Marekani Bi.Hillary Clinton amesema haiwezekani iwe kwamba hatakuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba. Katika mahojiano na kituo cha runinga cha CNN, amesema anajivunia uongozi mkubwa mbele ya mpinzani wake wa pekee Bernie Sanders. “Nitakuwa mgombea wa chama change,” ameambia CNN. “Hilo limekamilika tayari, kimsingi. Haiwezekani hilo lisitokee.” Bi …
EgyptAir: Mabaki ya Ndege Yatafutwa
Siku moja baada ya ndege ya shirika la Misri la EgyptAir kutoweka, vifusi vya ndege hiyo bado havijapatikana. Maafisa wa Misri wakisaidiwa na maafisa wa Ugiriki bado wanaendelea kutafuta vifusi hivyo katika bahari ya Mediterranean. Maafisa wa Misri awali walidhani kwamba vifusi vilivyopatikana vikielea kwenye bahari hiyo vilikuwa vimetoka kwa ndege hiyo, lakini baadaye ilibainika kwamba havikuwa vya ndege hiyo. …
Mtuhumiwa Ufisadi Akamatwa na Saa ya Thamani USD Milioni 1
POLISI wa kupambana na ufisadi nchini Nigeria, wamenasa saa yenye thamani ya takriban dola za Kimarekani milioni moja nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa zamani wa Wizara ya Mafuta Nigeria ambaye pia anachunguzwa kufuatia tuhuma za ufisadi. Saa hiyo ya kipekee ni moja kati ya vitu mbalimbali bvya mapambo ya dhahabu, almasi na fedha vilivyonaswa katika operesheni hiyo ya kushtukiza katika …
Hatutaongeza Muda wa Kuzizima Simu Feki – Waziri Mbarawa
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiiano Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali haitaongeza muda katika zoezi zima la uzimaji wa simu feki ifikapo Juni 16 mwaka huu. Ameyasema hayo ofisini kwake leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha habari hapa nchini. Amesema Serikali imeamua kuchukua uamuzi huo kutokana na madhara mbalimbali yatokanayo na simu hizo ikiwemo …
Obama Ajutia Makosa ya Marekani Dhidi ya Libya…!
RAIS wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilishindwa katika utatuzi mzozo wa Taila la Libya. Alisema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake. Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi. Alisema haya katika mahojiano na runinga …