MWENYEKITI wa Muungano wa Afrika, Thomas Boni Yayi, ametoa wito wa kutuma vikosi kusaidia wanajeshi kupambana na makundi ya wapiganaji nchini Mali. Wapiganaji hao ambao wanajumuisha wale wa Tuareg, wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi. ”Mzozo wa Mali ulikuwa kitendawili cha kimataifa na NATO inapaswa kusaidia kama ilivyo saidia Afrghanistan,” alisema Thomas Boni Yayi ”Hata hivyo, harakati dhidi ya wapiganaji …
Uchumi wa EAC Waimarika 2012 Licha ya Vikwazo Lukuki
Na Isaac Mwangi, EANA UCHUMI katika kanda ya Afrika Mashariki uliendelea kuimarika mwaka uliopita, 2012 licha ya changamoto lukuki iliyokabiliana nazo.Kanda nzima ilionyesha uchumi wake kukua kwa nguvu na kusukuma juhudi za kuimarisha mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). EAC inajumuisha nchi tano wananchama ikiwa ni pamoja na Kenya,Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi,Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki …
Wakuu 3 wa Polisi Wasimamishwa Kazi Kenya
MKUU wa polisi mkoani Rift Valley John M’mbijiwe anayedaiwa kuwa na uhusiano na mtu huyo mlaghai,John Waiganjo ingawa alikana kumfahamu Maafisa watatu waandamizi wa polisi nchini Kenya, wamesimamishwa kazi kuhusiana na sakata ya mtu mmoja ambaye aliwalaghai watu kuwa yeye ni naibu kamishna mkuu wa polisi kwa zaidi ya miaka mitano. Mkuu wa polisi mkoani Rift Valley John M’mbijiwe anayedaiwa …
Upinzani Ghana Wamsusia Rais Mahama
CHAMA rasmi cha upinzani nchini Ghana, kimesusia sherehe za kuapishwa kwa rais mpya John Mahama kufuatia uchaguzi wa mwezi jana uliokumbwa na utata. Chama cha New Patriotic Party (NPP) kilisema kuwa bwana Mahama hakushinda uchaguzi huo kihalali. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo, yalionyesha bwana Mahama akiwa na aslimia 50.7 idadi ambayo inatosha kuweza kuzuia duru ya pili ya uchaguzi dhidi …
Washukiwa wa Mapenzi ya Jinsia moja Waachiliwa huru
MAHAMAKA moja ya rufaa nchini Cameroon, imefutilia mbali hukumu dhidi ya watu wawili waliofungwa jela mwaka wa 2011, baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Wakili wawili Alice Nkom , amesema amefurahishwa na uamuzi huo kwa sababu jaji aliyetoa hukumu dhidi yao, alifanya hivyo chini ya shinikizo ya watu fulani. Mapenzi ya jinsia moja imeharimishwa nchini …
Rais wa Ghana aapishwa rasmi mjini Accra
Chama kikuu cha upinzani nchini Ghana, kimesusia sherehe za kuapishwa kwa rais John Mahama kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita uliokumba na utata. Chama cha New Patriotic Party (NPP) kimedai Bwana Mahama alishinda uchaguzi huo kwa njia ya udanganyifu. Matokeo rasmi yalimpa Bwana mahama ushindi wa asilimia 50.7, ya kura zaote zilizopigwa, kiwango ambacho kinamfanya kueouka duru ya pili ya uchaguzi …