VITUO vya kupiga kura vimefunga nchini Kenya katika mchakato mzima wa upigaji kura ya mchujo kote nchini. Katika baadhi ya maeneo ya Nairobi na viunga vyake uchaguzi ulikabiliwa na changamoto nyingi za maandalizi huku baadhi ya vyama vikilazimika kuakhirisha shughuli hiyo .Vyama vya siasa vinavyohusika hussusan muungano wa Cord unaoongozwa na waziri mkuu Raila Odinga havikuwa na mpangilio maalum na …
Wanajeshi Wajiandaa kwa Vita vya Ardhini Mali
Wanajeshi wa Ufaransa wanajiandaa kwa makabiliano yao ya kwanza muhumi ya ardhini wa wapiganaji wa waasi nchini Mali, baada ya kuanza safari hiyo kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Bamako. Msafara wa magari ya kivita 30 yaliondoka mjini Diabaly, takriban kilomita 350, Kaskazini mwa mji mkuu, mji ambao ulitekwa na wapiganaji hao waasi siku ya Jumatatu. Kikosi cha kwanza cha …
Al Shabaab kumuua Jasusi wa Ufaransa
WANAMGAMBO wa Al-Shabab nchini Somalia wanasema kuwa watamuua jasusi wa Ufaransa Denis Allex, ambaye Ufaransa ilisema kuwa alikuwa tayari ameuawa wakati jaribio la kumuokoa lilipotibuka. Walisema kuwa Ufaransa inapaswa kulaumiwa ikiwa atauawa. Na pia inapaswa kulaumiwa kwa mauaji ya makomando wengine wawili waliouawa Ijumaa katika msako uliofanywa mjini Bulo Marer. Maafisa nchini Ufaransa wanasema kuwa waliamini bwana Allex alikuwa ameuawa …
Wapiganaji Wauteka Mji Mwingine Mali
Wapiganaji wa kiisilamu walioteka Kaskazini mwa Mali Wapiganaji wa kiisilamu wameuteka mji uliokuwa unadhibitiwa na wanajeshi wa serikali licha ya harakati za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao kwa usaidizi wa Ufaransa. Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian alisema kuwa mji wa Diabaly, ambao uko umbali wa kilomita 400 kutoka mji mkuu ulitekwa katika makabiliano yaliyofanyika kati ya wapiganaji …
Mubarak Ashinda Kesi ya Rufaa
RAIS wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak, ameruhusiwa kufanyiwa kesi nyengine kwa makosa ya kutozuwia mauaji ya waandamanaji mamia kadha wakati wa ghasia zilizomuondoa madarakani. Mahakama ya rufaa mjini Cairo, baada ya kikao kifupi, yalitoa amri hiyo ya Bwana Mubarak kufanyiwa kesi nyengine. Mwezi wa Juni mahakama yalitoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa Rais Mubarak kwa hatia ya kuwa …
Mapigano ya Kikabila Yaendelea Kenya
WATU 11 wameuawa na wengine 15 kujeruhiswa mapema Alhamisi kwenye shambulio la kulipiza kisasi baina ya jamii mbili zinazohasimiana katika eneo la Tana River Delta. Shambulio linaifikisha 22 idadi ya watu waliouawa kwenye mapigano hayo ya kikabila yaliyozuka upya jana katika eneo la Nduru. Shambulio hili la alfijiri limetekelezwa katika kijiji cha Kibisu hatua chache tu kutoka eneno la Nduru …