Wapinzani Misri Wagomea Mazungumzo, Rais Atangaza Hali ya Hatari

KUNDI kubwa la upinzani nchini Misri limesema halitahudhuria mazungumzo yanayoandaliwa na Rais Mohamed Morsi hadi pale masharti yatakapotimizwa. Mkutano huo ulipanga kumaliza machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea katika miji kadhaa katika siku za hivi karibuni. Awali Rais Morsey alitangaza hali ya hatari ya muda wa mwezi mzima katika miji ya Port Said, Suez na Ismailiya kufuatia siku kadhaa ya maandamano na …

ECOWAS Kuongeza Vikosi Vyake Mali

MATAIFA ya Afrika Magharibi yamekubali kuongeza idadi ya wanajeshi wake watakaopelekwa Mali kuwaunga mkono wanajeshi wa nchi hiyo kupambana na waasi wenye itikadi kali za Kiislamu. Uamuzi huo umefikiwa wakati ambapo vikosi vya Mali na Ufaransa vikidhibiti maeneo muhimu ya Gao. Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi-ECOWAS waliokutana mjini Abidjan, Cote d’Ivoire wamefikia uamuzi huo ambapo sasa wanajeshi …

Kongamano la Kiuchumi la Davos Uswisi

PAMOJA na masuala ya kiuchumi wajumbe zaidi ya 2500 kwenye kongamano hilo la siku tano watajadili pia masuala ya ulinzi wa mazingira na ya maradhi. Wakuu wa serikali na viongozi wa nchi karibu 50 wanatarajiwa kulihudhuria kongamano la mjini Davos kwa lengo la kuhimiza matumaini na kuimarisha imani juu ya uchumi wa dunia, hasa wakati huu ambapo matumaini ya ustawi …

Uingereza Yatishia Kujitoa Umoja wa Ulaya

WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron ameonya kwamba ikiwa Umoja wa Ulaya hautafanya mageuzi ya msingi kupambana na matatizo yake, basi Uingereza itakuwa haina budi kutafuta njia za kujitoa kwenye Umoja huo. Akizungumza bungeni katika hotuba iliyopewa jina la “Uingereza na Umoja wa Ulaya”, Cameron ameahidi kwamba kufikia mwaka 2017 Uingereza itaitisha kura ya maoni kuwapa fursa raia wake kuamua …

ECOWAS Yaomba Isaidiwe Mali

VIONGOZI wa nchi za Afrika magharibi wameomba msaada wa kimataifa kugharimia majeshi yao kuingilia kati nchini Mali. Walisema hayo kwenye mkutano unaofanywa Abidjan, Ivory Coast. Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ambaye amehudhuria mkutano huo, ameshikilia kuwa majeshi ya Afrika yatashika uongozi wa operesheni za kijeshi nchini Mali katika majuma yajayo. Nchi kadha za Afrika …

Zebaki Kuacha Kutumika Duniani

NCHI zaidi ya 140 zimekubaliana kuchukua hatua za kuzuwia matumizi ya zebaki ambayo inachafua mazingira. Wajumbe katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva walikubaliana kupunguza, na hatimaye kumaliza kabisa, utumizi wa madini hayo yenye sumu ambayo inatumiwa kwenye zana kadha za majumbani kama zana za kupimia joto, yaani thermometers. Piya walikubaliana kupunguza zebaki inayotoka kwenye vinu vya nishati na …