Libya Washerehekea Mapinduzi ya Moammar Gaddafi

MAELFU ya watu walikusanyika katika miji miwili mikubwa nchini Libya, yaTripoli na Benghazi Februari 15, 2013 kusherehekea miaka miwili tangu kuanza kwa mapinduzi yaliyosababisha kuangushwa kwa Moammar Gaddafi. Katikati ya jiji la Tripoli, mamia yawatu walikusanyika katika uwanja wa mashahidi, wakipepea bendera na maputo na kuimba nyimbo za kusifu mashahidi waliokufa katika mapinduzi ya Libya wakati magari yakipita mjini wakipiga …

Mahakama Kuu Kenya Yatua ‘Mzigo’ Kesi ya Akina Ruto na Kenyatta

MAHAKAMA Kuu nchini Kenya imeeleza kwamba haiwezi kuamua iwapo Uhuru Kenyatta na William Ruto wanapaswa kugombea nyadhifa katika uchaguzi mkuu ujao. Wawili hao wanakabiliwa na tuhuma za kuchochea ghasia nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata na kusababisha mapigano ya kikabila. Ikiwa zimesalia wiki mbili tu kwa uchaguzi mkuu kufanyika Kenya, inaonekana kuwa wananchi ndiyo watakaoamua kupitia kura, iwapo …

Papa Benedict XVI Atangaza Kujiuzulu

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP. Katika taarifa yake, Papa amesema amefikia uamuzi huo ambapo sasa ana umri wa miaka 85. Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi …

Wagombea Urais Kenya Kupambana Katika Mdahalo

WAGOMBEA urais nchini Kenya wanatarajia kuumana katika mdahalo utakaowakutanisha viongozi hao na kuoneshwa moja kwa moja kupitia runinga. Mdahalo huo ambao ni wa kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo na unaotarajiwa kupima uwezo wa wagombea hao juu ya masuala muhimu ya kitaifa unafanyika wakati joto la kampeni likiwa juu hivi sasa. Mjadala huo ambao unafanyika baada ya juhudi za …

Watu 100 Wauwawa Sudan Kusini Baada ya Kushambuliwa

WAKUU wa Sudan Kusini wanasema watu zaidi ya 100 wameuwawa kwenye wizi wa mifugo. Taarifa zinasema watu wa kabila la Lou Nuer walishambuliwa Ijumaa katika Jimbo la Mashariki la Jonglei, huku taarifa zaidi zikidai shambilizi hilo lilifanywa na watu wa kabila la Murle. Umoja wa Mataifa (UN) unasema shambulio hilo ndio kubwa kabisa tangu mwaka wa 2011 ambapo watu wa …

Wauwawa Wakitoa Chanjo ya Polio Nigeria

RIPOTI kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa watu 12 wakiwemo wafanyakazi waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio kwa watoto, wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Maofisa wa afya nchini Nigeria wamewaeleza wanahabari kuwa wafanyakazi wanane waliokuwa wanatoa chanjo waliuawa mjini Kano na wengine kadhaa kujeruhiwa. Taarifa zaidi kutoka kwa watu walioshuhudia mauaji hayo zinasema kuwa, watu wengine 8 waliuawa katika kituo …