KIONGOZI wa Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika, Joachim Chissano ameishauri tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC kushirikiana na vyombo vya usalama kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa huru na haki. Chisano ambaye pia ni rais wa zamani wa Msumbiji ameyasema hayo mjini Nairobi katika mkutano wake na waandishi habari, baada ya kukutana na maafisa wa serikali, makundi ya …
Mkataba wa Kuleta Amani Kongo Watiwa Saini Ethiopia
MKATABA wa kumaliza vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo leo umetiwa saini mjini Addis Ababa-Ethiopia na viongozi wa nchi za Maziwa Makuu. Viongozi wa nchi za maziwa makuu leo mjini Addis Ababa wameutia saini mkataba wa kumaliza vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo uliofikiwa kwa upatanishi wa Umoja wa Mataifa. Viongozi hao walishindwa kuutia saini mkataba …
Watu 7 Wauawa Wakitoka Msikitini Kenya
WATU saba wameuawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi karibu na msikiti Kaskazini Mashariki mwa Kenya, karibu na mpaka na Somalia. Wanakijiji waliambia BBC kuwa watu kumi waliokuwa wamejihami waliwashambulia kwa bunduki watu hao wakati walipokuwa wanaondoka msikitini mapema asubuhi. Taarifa zinazohusiana Mwanzo wanaume watano waliuawa na kisha wanawake wawili waliosikia milio ya risasi walipofika kuchunguza, nao pia wakauawa. Shambulio linafanyika …
Pistorius Asema Alimuua Mpenzi Wake Pasipo Kujua
MWANARIADHA mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius alimuua mpenzi wake kimakosa baada ya kudhania kuwa alikuwa mwizi aliyekuwa amevamia nyumba yake. Aliiambia mahakama kuwa alimpenda mchumba wake Reeva Steenkamp na wala hakuwa na nia yoyote ya kumuua kama ilivyotokea. Viongozi wa mashtaka wanamtuhumu Pistoriusa kwa mauaji wakisema alikuwa amepnga kumuua mchumba wake baada ya kumpiga risasi mara tatu na kumuua …
EAC Yatuma Waangalizi wa Uchaguzi Kenya
JUMUIYA ya Afrika Mashariki imetuma kundi la waangalizi 40 watakaochunguza uchaguzi mkuu wa Kenya. Tayari wachunguzi 18 kutoka Muungano wa Ulaya waliwasili nchini humo mwishoni mwa Januari. Kundi hilo la waangalizi kutoka nchi zote wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki isipokuwa Kenya, litaanza kazi yake hivi leo likiongozwa na aliyekuwa spika wa bunge la Afrika Mashariki Abdurrahman Kinana kutoka Tanzania. …
Al-Shabaab Wamuua Mwanajeshi wa Kenya
KUNDI la Al-shabaab limesema kuwa limemuua mwanajeshi wa Kenya usiku wa Alhamisi, baada ya kumalizika kwa muda walitoa kwa serikali ya Kenya kuwaachia Waislamu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi. Wanamgambo hao wa Al-Shabaab wamesema pia kuwa wanachelewesha mauaji ya mateka wengine watano kwa masaa 72. Januari 23 wapiganaji hao waliipa serikali ya Kenya muda wa wiki tatu kuwaachia huru wapiganaji …