Kenya Wafanya Maamuzi ya Viongozi Wao

ZOEZI la upigaji kura nchini Kenya lililoanza saa 12 alfajiri leo 4.3.2013 bado inaendelea huku milolongo mirefu ya wapiga kura ikiendelea kushuhudiwa katika vituo mbali mbali. Lakini mauaji huko pwani yamelitia doa. Wagombea urais wakuu Uhuru Kenyatta na Raila Odinga tayari wamepiga kura zao huko Gatundu na Kibera mtawalia. Mwandishi wa DW mjini Nairobi Alfred Kiti anasema milolongo mirefu ya …

Amani Yazidi Kuhimizwa Uchaguzi Nchini Kenya

HUKU zoezi la upigaji kura likikaribia kuanza nchini Kenya, wagombea viti mbalimbali wamehimizwa kuzingatia kanuni za uchaguzi na kukubali matokeo ya uchaguzi huo ili kuepukana na kutokea kwa ghasia. Wito huo umetolea na kundi la waangalizi wa uchaguzi linalojiita “Group of Concerned Kenyans Initiative.”Kwenye mkutano na waandishi wa habari, kundi hilo likiongozwa na mwenyekiti wake, Generali Daniel Opande limesema limeridhishwa …

Obama Aidhinisha Makato ya Bajeti

RAIS Barack Obama wa Marekani ameidhinisha makato ya dola bilioni 85 katika bajeti ya serikali, ambayo yanaweza kuathiri uchumi wa nchi hiyo na kusababisha upotevu wa nafasi za ajira. Obama ameichukua hatua hiyo shingo upande, kutekeleza wajibu wake kisheria, ambao utaanzisha mara moja punguo katika bajeti ya kijeshi na matumizi ya ndani, baada ya kushindwa kupata makubaliano na chama cha …

Bosi wa IEBC Awataka wagombea Kuheshimu Matokeo ya Uchaguzi

Na Isaac Mwangi, EANA MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC), Ahmed Isaack Hassan ametoa wito kwa vyama vya siasa kuheshimu matokeo ya uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mapema wiki ijayo. Hassan alisema hayo alipokuwa anawapokea wakuu wa wajumbe wa Timu za Uangalizi wa Uchaguzi huo kutoka Taasisi Tatu za Kiuchumi za Kanda( RECs) waliomtembelea ofisni kwakeJumatano. Walifuatana na afisa mwandamizi …

Waumini Kanisa Katoliki Wamuaga Papa Benedikt wa 16, Awapa Ujumbe Mzito Makadinali

KIONGOZI wa kanisa katoliki ulimwenguni, Papa Benedikt wa 16 atakaestaafu kuanzia february 28 na kujishughulisha zaidi na ibada na kutafakari, ameongoza misa yake ya mwisho katika uwanja wa Mtakatifu Petro, wakihudhuria zaidi ya waumini laki moja na nusu kutoka kila pembe ya dunia.Wakaazi wa jimbo la kusini mwa Ujerumani Bavaria anakotokea kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni wamekuja kwa wingi …

Hatua za Lala Salama Uchaguzi wa Kenya

KINYANG’ANYIRO cha Uchaguzi Mkuu wa Kenya utakaofanyika Jumatatu kimeingia hatua ya lala salama hivi sasa, huku wagombea wakiendelea kuzunguka kwenye majimbo kuomba kura. Kura za maoni zinaonesha ushindani mkali upo kati ya mgombea Uhuru Kenyatta wa Jubilee na Raila Odinga wa CORD. Mshindani anayewafuata ni Musalia Mudavadi wa muungano wa Amani na anashikilia nafasi ya tatu nyuma ya wawili hao …