Kanisa Katoliki Lapata Papa Mpya, Ni Muagentina

RAIA wa Agentina, Cadinali Jorge Mario Bergoglio (76) amechaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa katoliki Duniani. Papa Mario Bergoglio ametangazwa usiku huu baada ya kumalizika kwa kikao cha uchaguzi cha Baraza la Makadinali wa Kanisa Katoliki duniani. Baba Mtakatifu, amejitokeza kwa mara ya kwanza kuwasalimu mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki waliokuwa wamekusanyika eneo la St. Peter Basilica, kumshuhudia kiongozi …

Hivi Ndivyo Uhuru Kenyatta Alivyombwaga Odinga

MWANA wa kiume wa muasisi wa taifa la Kenya, Uhuru Kenyatta, ameshinda uchaguzi wa rais kwa asilimia 50.07 ya kura kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi na hivyo kuepuka marudio ya uchaguzi. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Isaack Hassan Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amesema Kenyatta amejipatia asilimia 50.07 ya kura ambazo ni kura milioni 6.13 kulinganishwa …

Rais Kikwete Amtumia Salamu za Pongezi Rais Mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jayaka Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pongezi Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta. Katika salamu hizo zilizotumwa Jumamosi, Machi 9, 2013, saa chache baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Jumatatu, Machi 4, 2013, Rais Kikwete amemwambia Uhuru Kenyatta: “Mpendwa Rais Mteule …

Uchaguzi Kenya; Kenyatta Aongoza kwa 54% Odinga 41%

Na dev.kisakuzi.com Kenya; MATOKEO ya awali ya uchaguzi Mkuu nchini Kenya yameanza kutangazwa baada ya siku ndefu huku kura za awali zikionesha mchuano mkali upo kati ya Uhuru Kenyatta na kiongoza Raila Odinga. Hata hivyo hadi jana jioni Kenyatta kutoka muungano wa Jubilii alikuwa akiongoza kwa asilimia 54 huku mpinzani wake Odinga akimfuatia kwa asilimia 41. Hata hivyo Tume Huru …

Rais wa Venezuela Hugo Chavez Afariki

MAKAMU wa Rais wa Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kifo cha Rais Hugo Chavez (58) kufuatia kuugua kwa muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez alikuwa katika matibabu nje ya nchi yake kwa muda mrefu ambapo alikuwa akipatiwa matibabu yake nchi Cuba. Alirejea , mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza tangu maradhi yake yazidi kumsumbua na kupelekwa hospitali …

Rais Hugo Chavez Aaga Dunia!

Habari zilizotufikia mitamboni muda si mrefu, ni kwamba yule Rais machachari wa Venezuela kule America ya kusini amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani. Rais Chavez alikuwa anasumbuliwa na saratani kwa muda mrefu, na alikuwa akipelekwa Cuba kwa matatibabu mara kwa mara. Rais Chavez alifanikiwa kwa kiasi kukubwa kufanya ugonjwa wake siri na mapaka anafariki haikuweza kufahamika ni saratani ya …