RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara nyingine tena. Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo, ilisema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini muda mfupi kabla ya saa sita usiku. Mandela alilazwa siku kumi na nane hospitalini mwezi Disemba mwaka jana kupokea matibabu ya ugonjwa …
Serikali ya Marekani Yatumia Mil. $3.7 Mwaka 2012 Kugharamia Marais Wastaafu
WASHINGTON KUWA kiongozi wa dunia huru (the leader of the free world) ni mpango wenye gharama, na gharama zake hazikomi siku unapofungasha virago vyako kutoka Jumba Jeupe (White House). Serikali ya Marekani imetumia takribani Mil $3.7 mwaka jana kwa marais wake wastaafu, yaani, Jimmy Carter, George H.W. Bush, Bill Clinton, na George W. Bush (Maarufu kama Bush mtoto), hii imegundulika …
Waasi Wadaiwa Kuipinduwa Serikali Jamhuri ya Kati
WAASI wanadaiwa kuipindua serikali ya Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Kati, wamesema kwamba watasimamia serikali ya umoja wa kitaifa iliyopo, ikiwa na marekebisho madogo. Huku Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akisema wanajeshi 13 wa nchi yake wameuwawa katika mapigano nchini Afrika ya Kati walikokuwa wakipigana dhidi ya waasi. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa msemaji kutoka upande wa …
Rwanda Mwenyeji wa Mkutano wa Sayansi EAC
Na Mwandishi Wetu, EANA WATU wapatao 200 wakiwemo watafiti, wanasayansi na wapanga sera wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa nne wa Afya na Sayansi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mjini Kigali, Rwanda Machi 27-29, mwaka huu. Kauli mbiu ya mkutano huo wa siku tatu ni : Kipaumbele cha Kanda na matarajio:’’Ushahidi wa kuchukua hatua katika Changamoto za Mabadiliko ya Upatikana Fedha …
Mali: Mwanajeshi auwawa Timbuktu
MWANAJESHI mmoja wa Mali ameuwawa katika shambulizi la kigaidi katika mji wa kihistoria wa Timbuktu. Taarifa kutoka jeshi la Mali imesema kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na gaidi aliyekuwa ndani ya gari na amevalia kilipuzi. Dereva wa gari hilo alipofika katika kizuizi cha barabarani karibu na uwanja wa ndege alijilipua na kusababisha kifo cha mwanajeshi huyo mmoja. Hii ni mara ya …
Ntaganda: Kagame asema ataisaidia ICC
RAIS wa Rwanda Paul Kagame amesema kuwa atataoa masaada wa haraka kumsafirisha mshukiwa wa uhalifu wa kivita nchini DRC Bosco Ntaganda kwa mahakama ya kimataifa ya jinai, (ICC). Mshukiwa huyo anayejulikana kama “The Terminator”, alijisalimisha kwa ubalozi wa Marekani, Rwanda, Jumatatu. . Rais Kagame amesema kuwa Rwanda itawezesha kusafirishwa kwa mshukiwa huyo hadi Hague haraka iwezekanavyo. Generali Ntaganda amekuwa mhusika …