NCHI ya Afrika Kusini imetangaza kutuma wanajeshi Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kuungana katika kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa kilichoingilia kati nchini humo kuwanyan’ganya silaha wapiganaji. Taarifa ya kupeleka majeshi nchini Congo imetolewa ikiwa ni majuma machache baada ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati katika hali ya kutatanisha. Upande wa upinzani umelaani …
Waziri Marekani Atoa Sehemu ya Mshahara Wake kwa Wafanyakazi Serikalini
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry amesema atakuwa akitoa mchango wa asilimia tano ya mshahara wake kila mwaka, ili kuwanufaisha wafanyikazi wa Idara ya Serikali ya Marekani. Kerry sasa amejiunga pamoja na Rais wa Marekani, Barack Obama, na viongozi wengine wa Marekani kuonesha mshikamano na wafanyikazi wa serikali hiyo waliolazimika kuchukua likizo isiyokuwa na malipo kama hatua …
Marekati Kutoa Dola Mil. 5 Atakaye Fanikisha Kukamatwa Kony
MAREKANI imetangaza kitita cha Dola milioni 5 kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la waasi la Lord’s Resistance Army LRA, la nchini Uganda, ambaye ni mmoja wa watu wanaotafutwa sana duniani. Tangazo hilo la Marekani limekuja siku moja tu baada ya Uganda na Washington kusema kuwa wamelazimika kusitisha msako wa miaka miwili wa mbabe huyo wa kivita katika misitu …
Korea Kaskazini Yaendeleza Vitisho
HALI ya wasiwasi imezidi katika rasi ya Korea baada ya Korea Kaskazini kufunga maeneo muhimu yanayounganisha eneo la viwanda na Korea Kusini, huku Urusi na China zikiitaka Korea kusitisha zoezi hilo. Wasiwasi huo unakuja baada ya Korea Kaskazini kufunga mipaka yake ya kijeshi iliyopo umbali wa kilomita 11 upande wa Kaskazini, na kuzuia zaidi ya Wafanyakazi 861 wa Korea Kusini …
Vikosi vya Umoja wa Ulaya Vyaanza Kuwajibika Nchini Mali
WANAJESHI wa Umoja wa Ulaya wanaanza kuwapatia mafunzo wanajeshi wa Mali katika wakati ambapo opereshini za kijeshi zinazoongozwa na Ufaransa zinaendelea katika mji wa kaskazini wa Timbuktu. Kouli Koro ni mji unaokutikana umbali wa saa moja kwa gari kutoka mji mkuu wa Mali-Bamako.Huko ndiko wanajeshi wa Umoja wa Ulaya walikopiga kambi yao-mbali kabisa na uwanja wa apigano, kaskazini ya Mali. …
Uchaguzi Kenya Ulikuwa Huru na wa Haki -Mahakama
MAHAKAMA ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki. Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane. Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama …