Milipuko Yaitikisa Boston Marathon, Yajeruhi Kadhaa

MILIPUKO miwili katika eneo la kukamilisha mbio ndefu za Boston imesababisha majeruhi wasiojulikana idadi yao. Picha na video kutoka Boston zinaonyesha watu wakiwa wamechanganyikiwa wasijue pa kwenda, huku magari ya huduma za dharura yakielekea katika eneo la tukio na watu waliojeruhiwa vibaya wakipelekwa kwenye hema la matibabu ya haraka. “Kuna watu wengi wamelala chini,” alsiema mwanariadha mmoja akinukuliwa na chombo …

Vicheko vya Matumaini?

Ni matumaini yetu kwamba waheshimiwa kwenye picha hapo hawacheki kwa unafiki, bali ni kwa mapenzi ya nchi yao ya Kenya. Wahenga walisema “Asiyekubali kushindwa si mshindani”, hivyo basi, tunafarijika kuona Kambi ya upinzani ya chama cha CORD kinachoongozwa na Mh. Raila Odinga kimekubali kushindwa na kimetaka Wakenya wasonge mbele kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya Kenya. Pichani, ni Mh. Uhuru …

Bashir Aamuru Mipaka ya Sudan Kufunguliwa

RAIS Omar al-Bashir wa Sudan, katika ziara yake ya kwanza mjini Juba tangu nchi ya Sudan ya Kusini kuwa huru mwaka 2011, ametangaza mipaka kati ya nchi hizo mbili kufunguliwa. Akizungumza akiwa na rais mwenzake, Salva Kiir, Bashir alitaka pia mataifa hayo mawili kudumisha amani, na kuimarisha uhusiano wa kawaida tena. Hali ya uhasama iliongezeka kati ya mataifa hayo mawili …

Uganda Kuwa Mwenyeweji Mafunzo ya Kijeshi ya EAC

Na James Gashumba, EANA UGANDA itakuwa mwenyeji wa mafunzo ya tatu ya kijeshi ya kanda ya Afrika Mashariki mwezi ujao yatakayojumuisha askari 1250 ikiwa ni sehemu ya jeshi litakalokuwa tayari kwa dharura yoyote katika kanda ifikapo 2015, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti. Kikao maalum cha 9 cha Baraza la Mawaziri wa Ulinzi na Usalama wa Kanda …

Rais Kagame Ataka Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari Washitakiwe

Na James Gashumba, EANA RAIS wa Rwanda, Paul Kagame ametoa wito kwa nchi ambazo bado zinawahifadhi watuhumiwa wa mauaji ya kimbari kuwarejesha nchini Rwanda au kuwafungulia mashitaka, linaripoti Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA). “Tunashukuru kwamba baadhi ya nchi zimeaanza kufuatilia na kuwatia mbaroni watuhumiwa wa mauaji ya kimbari waliopo nchini mwao, na wengie wamesharejeshwa nchini Rwanda.Hata hivyo …

Uhuru Kenyata Aapishwa Rasmi Kuiongoza Kenya

ALIYEKUWA Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Kenya na kukabidhiwa madaraka na rais aliyemaliza muda wake, Mwai Kibaki. Kenyata amekula kiapo rasmi katika Uwanja wa Taifa la Kenya wa Moi Kasarani kwa kutumia biblia ambayo aliitumia Baba yake alipokuwa madarakani. Kiapo cha Kenyata ambaye ni rais wa nne kimehudhuriwa na marais mbalimbali kutoka nchi …