Ubalozi wa Ufarasa Washambuliwa kwa Bomu Nchini Libya

SHAMBULIO la bomu lililotegwa ndani ya gari karibu na Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Mjini Tripoli nchini Libya limewajeruhi watu 2 na kusababisha hasara kubwa baada ya kulipuka. Hili ni shambulio la kwanza dhidi ya masilahi ya Ufaransa nchini humo. Shambulio hilo linalotajwa kuwa ni la ‘kigaidi’ na viongozi wa Serikali ya Libya, limejiri katika wakati ambapo hali ya usalama …

Watatu Wauwawa, Milipuko ya Boston, Marekani, 140 Wajeruhiwa

HADI sasa watu watatu wameshakufa kutokana na mashambulio ya mabomu mawili yaliyolipuka wakati wa mbio ndefu za marathon katika Mji wa Boston nchini Marekani, Mabomu mawili yalilipuka kwenye mitaa iliyokuwa imejaa watu karibu na sehemu ya kumalizia mbio za marathon. Watu watatu wamekufa kutokana na milipuko ya mabomu hayo yaliyoutikisa Mji wa Boston, Jimbo la Marekani la Massachusettes. Milipuko hiyo …

Polisi Mogadishu Waanza Msako Kutafuta Wauaji wa Zaidi ya Watu 35

POLISI nchini Somalia wameanzisha msako mkubwa kutafuta silaha, ikiwa ni siku moja baada ya mashambulizi makubwa kutokea mjini Mogadishu na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 35. Ofisa mkuu wa polisi nchini Somalia, Mohammed Hassan, amesema kwa sasa watu zaidi ya 400 wamekamatwa katika oparesheni hiyo ambayo inanuia kuimarisha usalama. Jana Jumapili watu tisa waliokuwa wamevalia mikanda ya mabomu walijiripua …