RAIS WA UGANDA Yoweri Museveni amefanya mabadiliko katika makamanda wake wakuu wa jeshi , huku kukiwa na taarifa za kutofautiana kwa majenerali wa jeshi kuhusu ikiwa mwanawe Museveni anaweza kumrithi babake kama rais. Mkuu wa majeshi, Aronda Nyakairima aliyetajwa katika taarifa iliyofichuliwa kuwa mmoja wa wanaopinga mwanawe Museveni Muhoozi Kainerugaba kumrithi babake, amehamishwa hadi wadhifa wa kiraia kuwa waziri wa …
Nchi za Afrika zashauriwa kuwaenzi diaspora
Na Hassan Abbas, Addis Ababa Viongozi wa Afrika wametakiwa kuenzi mchango wa Waafrika walioko nje ya Bara na walioko nje ya nchi zao si tu kwa kutambua mchango wao kiuchumi bali kuwapatia haki za kiraia na kisiasa ikiwemo kupiga kura. Wito huo umetolewa jijini hapa wakati wa mkutano wa siku mbili ulioandaliwa kutafakari miaka kumi ya Mpango wa Afrika Kujitathmini …
Benki ya Dunia Kutoa Bil 1 Kusaidia Nchi za Maziwa Makuu
BENKI Kuu ya Dunia itatoa dola bilioni 1 kusaidia maendeleo ya eneo la maziwa makuu. Rais wa Benki hiyo Jim Yong Kim ameyasema hayo mjini Kinshasa alikowasili akiandamana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon. Akizungumza mjini Kinshasa, Rais wa Benki Kuu ya Dunia Jim Yong Kim amesema kuwa fedha hizo zitakazotolewa na benki anayoiongoza zitatumika kuboresha …
Raia Waachwa Nje ya Mchakato wa Mtangamano wa EAC-Utafiti
Na Mtuwa Salira, EANA Arusha MATOKEI ya kwanza ya utafiti juu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umeonyesha kwamba jumuiya hiyo iliundwa kama chombo kilichoandaliwa kuwepo kwa maslahi ya serikali na wafanyabiashara wakubwa. Jumuiya hiyo yenye wananchama watano ingawa ilianzishwa upya kuwa ‘’jumuiya yenye misingi ya watu’’ wenyewe wa Afrika Mashariki, imebainika ushiriki wa raia wa kawaida katika mchakato wa …
Obama Kuzuru Afrika, Mashambulio Iraq 95 Wauwawa
RAIS wa Marekani anatarajiwa kuzuru Bara la Afrika mwezi ujao ambako atazuru mataifa ya Senegal, Afrika kusini na Tanzania. Katika taarifa msemaji wa Ikulu ya Rais Jay Carney amesema Obama anapangiwa kufanya ziara hiyo kati ya tarehe 28 mwezi ujao hadi tarehe 3 mwezi Julai ambako atakutana na viongozi wa serikali, biashara na wa mashirika ya kijamii kwa lengo la …
Polisi Uganda Wavamia Ofisi za Vyombo vya Habari Kusaka Kielelezo
POLISI nchini Ugandan wamevamia ofisi za magazeti kufuatia taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais. Taarifa zinasema vituo viwili vya Redio pia vilivamiwa limeandika Gazeti la Serikali la New Vision. Wiki iliyopita magazeti ya Uganda yalidai kuwa zipo njama za kuwaua wale watakao pinga mpango wa Rais Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda. Magazeti hayo …