HATIMAYE mwana mama Theresa Mary May amechukua usukani na kuwa Waziri Mkuu wa taifa la Uingereza. Akizungumza baada ya kupokea ufunguo wa makao rasmi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. May amewahakikishia washirika wake na mataifa ya muungano wa ulaya kuwa licha ya taifa hilo kuamua kujiondoa, Uingereza imedhamiria kuungana na mataifa washirika na kutekeleza wajibu wake katika muungano wa …
NMB Yawajaza Mapesa Washindi wa Pata Patia Maonesho ya Sabasaba
BENKI ya NMB imetangaza washindi wa droo nyingine ya mchezo wa bahati nasibu wa Pata Patia na kuwajaza mpesa washindi watatu wa mchezo huo katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere eneo la Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Zoezi la kuwakabidhi zawadi hizo lililofanyika ndani ya Banda la NMB ‘Sabasaba’ …
Ubaguzi wa Rangi: Mnigeria Auawa Italia
Polisi nchini Italia wamemtia mbaroni mwanamme mmoja anayeshukiwa kumpiga hadi kufa mhamiaji mmoja raia wa Nigeria katika shambulizi la kibaguzi kwa misingi ya rangi. Emmanuel Chidi amekuwa akiishi Italia tangu mwaka wa 2015, baada ya kutoroka vita nchini Nigeria. Emmanuel Chidi alivamiwa siku ya jumanne alasiri katika mji Fermo alipokuwa akitembea na mkewe. Ripoti zinasema raia mmoja wa Italia alimtusi …
Wayahudi wa Ethiopia Kupelekwa Israel
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema serikali yake itaendelea na mpango wa kuwahamishia Wayahudi wa Ethiopia hadi nchini Israel. Amesema serikali yake itahakikisha Wayahudi waliokwama nchini Ethiopia wanasafiri kujiunga na jamaa zao ambao tayari wamefika Israel. Takriban Waethiopia 9,000 wanaodai kuwa Wayahudi wanasubiri kuhamia Israel, na wamesubiri kwa miaka mingi. Akihutubia wanahabari mjini Addis Ababa, bw Netanyahu amesema shughuli …
Waziri Mkuu wa Uingereza Atangaza Kujiuzulu
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya. Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke. Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani. …
Maalim Seif Hamad Ahitimisha Ziara Marekani, Aelekea Canada.
Na Mwandishi Wetu Washington MAKAMU wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, jana alimaliza ziara yake nchini Marekani iliyochukua muda wa wiki moja. Maalim Seif alikhitimisha ziara yake hiyo kwa mkutano wa hadhara ambapo alipata nafasi ya kuongea na Watanzania waishio nchini humu. Katika Mkutano huo, mwanasiasa huyo gwiji nchini …