Jeshi Lampinduwa Rais wa Misri, Mohammed Morsi, Obama Apongeza

MVUTANO kati ya mamilioni ya waandamanaji na Rais wao, Mohammed Morsi sasa umefikia tamati baada ya Jeshi la nchi hiyo kuamua kumpinduwa rais Morsi kwa kile ushindwa kupata suluhu kwa muda aliopewa na jeshi. Hata hivyo kabla ya hatua ya kupinduliwa Rais Morsi alihutubia na kusisitiza kuwa hatong’atuka madarakani kama walivyokuwa wakidai mamilioni ya waandamanaji wanaompinga. Hali ya wasiwasi ilitanda …

Hali si Shwari Tena Nchini Misri

MISRI inaadhimisha mwaka mmoja wa Rais Mohammed Musri madarakani kwa siku nyengine ya maandamano ya umma ambapo wapinzani wamedhamiria kumuondoa madarakani na wale wanaomuunga mkono wakiapa kumlinda hadi mwisho. Vuguvugu la Tamarod, jina la Kiarabu linalomaanisha uasi, ndilo linaloendesha kampeni ya kumng’oa Rais Mursi likidai kuwa limeshakusanya saini milioni kadhaa zinazounga mkono kampeni yao na kuitishwa uchaguzi mpya. Mabango yanayowataka …

Obama Awaonya Viongozi Afrika, Akutana na Familia ya Mandela

RAIS Barack Obama wa Marekani akiwa katika ziara yake Afrika Kusini ameshauri viongozi wa Afrika na duniani kwa jumla kufuata mfano wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela kwa kulitanguliza mbele taifa kabla ya nafsi yake. Obama alisema kama viongozi wanashikilia nyadhifa hizo kwa muda na wasidanganyike kiasi cha kufikiri kwamba hatima ya nchi yao haitegemei kadiri watakavyoendelea …

Wageni Wamiminika Nyumba ya Mandela, Soweto

WATOTO wa shule, wafanyabiashara na watalii kutoka duniani kote, ikiwa ni pamoja na Wajerumani, wanamiminika kwenye nyumba ya zamani ya mzee Nelson Mandela katika kitongoji cha Soweto kumtakia afya njema. Hali ya Mandela yasemekana imekuwa nzuri kidogo japokuwa bado yu chumba cha wagonjwa mahututi. Wakati Mandela mwenyewe amelazwa hospitalini bado akiwa katika hali mbaya, watoto wa shule wa Afrika Kusini, …

Nelson Mandela yu Mahututi…!

WANANCHI wa Afrika Kusini wanaelekea kazini asubuhi ya leo wakiwa na simanzi huku wakisubiri habari zaidi kuhusu afya ya rais wao mstaafu Nelson Mandela ambaye madaktari wanasema hali yake ni mahututi. Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika Kusini zilisema Jumapili jioni kuwa Mandela alikuwa amezidiwa ingawa madaktari wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa anapata afueni. Taarifa kutoka kwa ofisa mmoja mkuu alisema …

Rais Barack Obama Aacha Gumzo Berlin

AKIKUMBUSHIA historia kali ya Mji wa Berlin uliyogawika wakati mmoja, Rais Barack Obama amezitahadharisha Marekani na Ulaya dhidi ya kuridhika kunakosababishwa na amani, huku akiapa kupunguza silaha za nyuklia. Rais Obama pia alitangaza kuwa programu yake ya udukuzi wa mawasiliano iliyozua zogo duniani, imenusuru maisha katika pande zote za Atlantiki. Akihutubia umati uliokusanyika katika lango kuu la Brandenburg, Obama alisema …