Baada ya Walimu Kugoma Kenya, Wanafunzi Wagida Pombe Baa

POLISI wa Kenya wamewakamata zaidi ya wanafunzi elfu moja baada ya kupatikana wakiwa walevi mjini Nairobi wikendi hii. Polisi waliendesha msako katika baa anuai na vilabu vya burudani baada ya kupokea malalamishi kwamba watoto wa shule wamekua wakifurika kwenye burudika tangu mgomo wa walimu uanze. Taarifa zinasema kwa sasa wanafunzi wengi hawako shuleni baada ya waalimu wa Kenya kugoma wakitaka …

Familia ya Mandela Washikana Ugoni

*Mandla amtuhumu Mbuso kuzaa na mkewe CHIFU Zwelivelile Mandlesizwe Dilubhunga ‘Mandla’ Mandela (39), ambaye ni mjukuu mkubwa wa kiume wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amemtuhumu mdogo wake, Mbuso Mandela (22) kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe. Tuhuma hizo nzito ndani ya familia ya Mandela, zimeibuliwa na Mandla kwa kumtaja jina moja kwa moja Mbuso kuwa …

Moyo wa Mandela Ulisimama – Daktari

KUHARIBIKA kwa gari la wagonjwa lililombeba Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kulisababisha moyo wa shujaa huyo kusimama kwa dakika 40. Hayo yalibainishwa na daktari wa moyo anayemtibu shujaa huyo wa Afrika Kusini, kwamba Juni 8, mwaka huu, wakati akipelekwa hospitali gari lililombeba lilipata hitilafu njiani na kukwama kwa muda. Daktari huyo wa moyo anayeheshimika nchini Afrika Kusini, …

Mandela Aikoroga Afrika Kusini

*Mjukuu ataka Winnie, Graca wasiingilie ukoo *Askofu Tutu, Zuma, Makamu wa Rais waingilia SASA kuna dalili kuwa familia ya rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, imeparaganyika kutokana na ugomvi kuhusu eneo la makaburi. Mandla Mandela, mjukuu mkubwa wa kiume wa Mandela ambaye juzi alishindwa kesi aliyokuwa amefunguliwa na shangazi yake, Makaziwe Mandela, ya kuvamia eneo la makaburi …

Rais wa Muda wa Misri Aapishwa

JAJI Mkuu wa Mahakama ya Juu zaidi ya kikatiba ameapishwa nchini Misri kuwa rais wa muda baada ya jeshi kumng’oa madarakani rais aliyechaguliwa na raia kwa njia ya kidemokrasia na kushinda kwa wingi wa kura, Mohammed Morsi. Viongozi duniani wamepokea kwa tahadhari matukio yanayojiri huko Misri. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amewaambia waandishi kwamba anaangalia kwa …

Mjukuu wa Mandela Ashindwa Kesi ya Makaburi

MJUKUU wa Mzee Nelson Mandela, Mandla Mandela ameshindwa kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yake kwa tuhuma za kufukua makaburi ya jamaa za familia yake katika mzozo wa makaburi uliozua utata ndani ya familia ya Mandela. Mgogoro huo unahusu maiti za wanawe Mandela watatu ambao Mandla alihamisha na kuwazika karibu na nyumbani kwake zaidi ya miaka miwili iliyopita. Taarifa zinasema Mahakama Kuu …