Mwanamke Aliyepotea kwa Miaka 50, Apatikana Kikongwe

MWANAMKE mmoja aliyepotea kwa zaidi ya miaka 50 mjini Surrey, Columbia amepatikana akiwa hai na kikongwe huku akiwaacha na maswali waliompata kutokana na hali aliyokuwa nayo kwa sasa. Mwana mama huyo, Lucy Johnson (77) alipotea akiwa na mumewe, Marvin Johnson tangu mwezi Mai, 1965 na taarifa kuripotiwa polisi wa mji huo kwa uchunguzi zaidi. Hata hivyo baada ya juhudi za …

Rais Sudan Kusini Avunja Baraza la Mawaziri

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amelivunja Baraza lake la Mawaziri pamoja na kumfukuza kazi, Makamu wa Rais Riak Machar katika mabadiliko makubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika historia ya miaka miwili ya taifa la hilo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Barnaba Marial Benjamin, ameliambia Shirika la Habari la BBC kuwa mawaziri wote kutoka upande wa …

Waasi M23 wadaiwa Kubada na Kuuwa DRC

SHIRIKA la kutetea haki za Binadamu la ‘Human Rights Watch’ limesema kuwa kundi la wapiganaji la M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrsia ya Congo limewaua zaidi ya watu 40 na kuwabaka zaidi ya wanawake na wasichana 60 tangu Machi mwaka huu. Taarifa hizo zimepatikana baada ya shirika hilo kuwahoji zaidi ya watu 100 eneo hilo. Shirika hilo limesema licha ya …

SADC Yatarajia Uchaguzi Huru na Haki Zimbabwe

KAMATI ya Siasa Ulinzi na Usalama ya nchi zinazounda Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) imesema ina imani kuwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini Zimbabwe utakuwa huru na wa haki. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo juzi tarehe 20 Mjini Pretoria mara baada ya kumalizika kwa kikao cha siku moja cha kamati ya SADC iliyokutana …

Uchaguzi Mkuu Zimbabwe Kuwa Mgumu – SADC

VIONGOZI kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Julai 20, 2013 wameonya kuwa utayarishaji wa Uchaguzi Mkuu wa Zimbabwe utakuwa mgumu kutokana na muda mfupi wa maandalizi uliowekwa. Mataifa 15 wanachama wa SADC mwezi uliopita uliitaka Zimbabwe kusogeza mbele uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Julai 31 kwa wiki mbili zaidi ili kuruhusu muda wa kutosha kuweza kutekeleza …

Umoja wa Mataifa Kupeleka Jeshi la Mapambano Congo

UMOJA wa mataifa umesema upo tayari kupeleka jeshi katika uwanja wa mapambano huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kukabiliana na waasi. Hatua hiyo inayotokana na malalamiko ya wananchi walio andamana mjini Goma wakilalamika. Waandamanaji hao walilalamikia kitendo cha walinzi wa amani kutowasaidia majeshi ya Serikali kukabiliana na vitendo vya waasi maeneo hayo. Jeshi la Umoja wa Mataifa (UN) …