UWANJA wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta umefungwa kwa muda baada ya moto mkubwa kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi. Kwa sasa moto huo unaendelea kudhibitiwa na vyombo husika. Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja huo na anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari baadaye. Hadi kufikia sasa hakuna ripoti zozote za majeruhi zimetokea kufuatia tukio la moto …
Tsvangirai Kufungua Kesi Kupinga Matokeo ya Uchaguzi
SIKU moja baada ya Rais Robert Mugabe na Zanu PF kutangazwa kushinda Uchaguzi Mkuu nchini Zimbabwe, baadhi ya wafuasi wa upinzani kutoka chama cha MDC wanasema wameshambuliwa na wenzao wa ZANU PF. Baadhi ya dola za Magharibi ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, zimetilia shaka iwapo uchaguzi huo ulifanyika kwa uwazi. Madai hayo yanakuja siku moja baada ya matokeo …
Mugabe Ambwaga Tsvangirai Uchaguzi Mkuu Zimbabwe
RAIS Jacob Zuma wa Afrika Kusini amempongeza Robert Mugabe (89) kwa kuchaguliwa tena kuiongoza Zimbabwe, baada ya kumshinda mpinzani wake Morgan Tsvangirai katika muhula wa saba wa uongozi wa taifa hilo. Rais Zuma amesema uchaguzi mkuu wa Zimbabwe ulifanikiwa, na ametoa wito kwa pande zote zikubali matokeo. Mpinzani mkuu wa Bwana Mugabe, Morgan Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 61, amekataa …
Mugabe Ahaidi Kung’atuka Akishindwa Uchaguzi
RAIA wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa miaka 89 amesema atang’atuka ikiwa yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa. Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili kunyakua ushindi, …
Papa Francisco Awataka Wakristu Kutopenda Mali na Madaraka
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francisco, amewataka Wakristu Wakatoliki kuachana na kile alichokiita kupenda mali na madaraka. Wito huo ameutoa wakati akiadhimisha Ibada ya Misa katika Pango Takatifu huko Aparecida, kwenye Jimbo la Sao Paulo nchini Brazil. Akihubiri wakati wa Ibada ya Misa yake ya kwanza kuadhimisha tangu awasili Brazil, katika Kanisa Kuu la Madhabahu ya Mama Bikira …
Mbakaji Maarufu Ajinyoga Gerezani
MWANAMUME anayetuhumiwa kwa makosa mengi ya umbakaji, ‘mbakaji sugu’ nchini Afrika Kusini, Sifiso Makhubo, amekutwa akiwa amefariki katika chumba chake gerezani. Sifiso Makhubo, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka 122 yakiwemo ya mauaji na ubakaji amekutwa akiwa amekufa huku ikiaminika amejinyonga kwa kutumia blanketi alilokuwa nalo katika chumba chake. Baadhi ya makosa aliyoshtakiwa nayo Makhubo ni pamoja na kuwaambukiza virusi vya HIV …