RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe ameyaonya mataifa ya Marekani na Uingereza na kuzitaka ziondoe vikwazo dhidi ya nchi yake, ama sivyo Zimbabwe italipiza kisasi. Alisema hatua zao ni sawa na kusimbuliwa, na alisema wakati utafika kwa Zimbabwe kuchukua hatua za kujibu. Rais Mugabe alisema hayo katika mazishi ya afisa wa jeshi la wanahewa. Hivi karibuni viongozi wa SADC walipokutana nchini …
Maofisa 24 wa Polisi Misri Wauwawa, Mohammed Badie Akamatwa
TAKRIBAN maofisa 24 wa Polisi nchini Misri wameuawa kwenye shambulizi la kushtukiza katika eneo la Rasi la Sinai. Taarifa zinasema polisi hao walikuwa kwenye msafara wa mabasi mawili yaliyoshambuliwa na kundi la watu waliokua na silaha karibu na Mji wa Rafa mpakani na Ukanda wa Gaza. Polisi watatu walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Hivi karibuni jeshi la Misri limeimarisha operesheni dhidi …
Wanamgambo Wawauwa Polisi kwa Risasi Kenya
WANAMGAMBO wa kisomali wamewauawa kwa kuwapiga risasi polisi wanne wa Kenya karibu na mpaka wa Somalia, maofisa wamesema. Takriban watu 40 waliojihami kwa silaha walishambulia kituo cha Polisi juzi, kamishna wa kaunti hiyo amesema. Kundi la alshabaab limethibitisha kufanya shambulio hilo. Kenya imekumbwa na msururu wa mashambulio tangu majeshi yake yaingie kusini mwa Somalia kukabili wapiganaji wa Alshabaab mwaka wa …
Michel Djotodia Aapishwa Kuwa Rais
KIONGOZI wa zamani wa waasi ambaye alifanya mapinduzi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia ameapishwa kuwa rais. Djotodia ameahidi kuandaa uchaguzi kufikia mwanzo wa mwaka ujao. Tangu achukue uongozi mwezi Machi kupitia kikundi cha waasi wa Seleka nchi hiyo imetajwa kutumbukia zaidi katika umaskini na utovu wa sheria. Shirika la Umoja wa mataifa linakadiria kuwa zaidi ya theluthi …
Oprah Winfrey ‘Adhalilishwa’ Switzerland
MWANAMKE maarufu duniani, Oprah Winfrey amekumbana na kitendo cha ubaguzi wa rangi nchini Switzerland baada ya muuza duka mmoja kukataa kumuuzia mkoba wa kike wa mkononi na kumwambia kuwa asingeweza gharama yake. Oprah ambaye ametajwa katika vitabu vya ‘Forbes’ kama mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa duniani na mmoja wa watu matajiri zaidi amedai kuwa muhudumu wa kisichana aliyekuwa akiuza …
MDC Wamfikisha Robert Mugabe Mahakamani
CHAMA cha Movement for Democratic Change (MDC) nchini Zimbabwe kimewasilisha malalamiko yake mahakamani kupinga ushindi wa Robert Mugabe katika uchaguzi wa rais wa wiki iliyopita. MDC inataka matokeo ya uchaguzi huo yabatilishwe na uchaguzi mpya uitishwe katika kipindi cha siku 60. Chama hicho kimetaja mambo 15, mkiwemo madai ya kutoa hongo, kutumia vibaya haki ya kuwasaidia wapigaji kura na kuvuruga …