RAIA mmoja wa nchi ya Canada amekamatwa nchini Colombia baada ya kujaribu kupanda ndege kurejea Canada akiwa na tumbo bandia la ujauzito alimokuwa ameficha dawa za kulevya aina ya Cocaine. Mwanamke huyo aliyekuwa anajifanya kuwa mtalii akirejea Toronto, alihojiwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Bogota aliyemshuku na kumuuliza alikuwa amesalia na miezi mingapi kujifungua. Alijibu kwa ukali mno, …
William Ruto Aifuata Kesi Yake The Hague
MAKAMU wa Rais wa Kenya William Ruto anakwenda The Hague, Uholanzi, ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kesi inayomkabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Binaadamu (ICC) mjini humo. Ruto mwenye umri wa miaka 46 anakabiliwa na mashitaka ya kuandaa machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 ambapo mamia ya watu waliuwawa. Kiongozi huyo ni mwanasiasa …
G20 Watofautiana Kuhusu Syria, Papa Ataka Yafanywe Maombi ya Amani
MKUTANO wa viongozi wa nchi 20 zinazoongoza kiuchumi duniani, G20 umefanyika Septemba 6, 2013 huku viongozi hao wakitofautiana kuhusu mzozo wa Syria na Baba mtakatifu Francis akitoa wito wa maombi ya amani. Mkutano wa viongozi wa nchi 20 zinazoongoza kiuchumi duniani, G20 umekamilika 6, 2013 huku viongozi hao wakiwa wametofautiana kuhusu mzozo wa Syria. Rais wa Urusi Vladimir Putin alidhihirisha …
Mohammed Morsi Afunguliwa Mashtaka ya Uchochezi
KIONGOZI wa mashtaka nchini Misri, amependekeza kuwa aliyekuwa Rais Mohammed Morsi afunguliwe mashtaka kwa kosa la kuchochea mauaji ya waandamanaji. Tuhuma hizo zinahusiana na ghasia zilizotokea nje ya ikulu ya rais mjini Cairo Disemba mwaka jana ambapo angalau watu saba waliuawa kwenye makabiliano. Wanachama wengine 14 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood pia wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka kuhusiana na makosa hayo hayo. …
Rais Obama Aomba Bunge Kuidhinisha Vita, Mandela Atoka Hospitali Akiwa Mahututi
HAIKUSADIKIKA kuwa Marekani itachukua hatua za haraka za kijeshi dhidi ya Syria, baada ya Rais Barack Obama wa nchi hiyo kuliomba bunge lake kuidhinisha shambulio. Kwa sasa Bunge halitaanza tena vikao vyake hadi Septemba 9, 2013. Mswada huo uliowasilishwa unaomba idhini ya bunge kutumia nguvu kuizuia serikali ya Syria kutumia silaha za kemikali kwenye mashambulio. Kuchelewa kwa ratiba ya Marekani …
Watoto Wanyanyaswa Kingono Migodini Tanzania
SHIRIKA la haki za binaadamu la Human Rights Watch limechapisha ripoti inayoelezea mazingira magumu wanayokumbana nayo watoto wanaojiingiza kwenye ajira ya uchimbaji madini nchini Tanzania, wengi wao wakiathirika kiafya. Ikiwa na kichwa cha habari kisemacho “Ajira ya Watoto katika Migodi”, ripoti hiyo imefichua vitendo vya dhuluma na ukatili wanaokutana nao watoto wao ambao baadhi yao wako hatarini kuangukia kwenye matatizo …