Ujerumani Wajenga Jumba la Mwalimu Nyerere, AU

  KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jumba jipya la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la Rais wa Kwanza wa Taifa la Tanzania, Julius Nyerere. Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka nchini Ujerumani. Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU …

Atakaye Kaidi Kufanya Usafi Tanga Kustakiwa..!

  MWENYEKITI wa mtaa wa Centrol Tanga, Diana Mussa, amewataka wakazi wa eneo hilo kuweka mazingira ya usafi kwa kila nyumba ili kuondosha kitisho cha magonjwa ya milipuko na kusema kuwa ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria. Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa duka la kuuza umeme la Zola lililopo barabara ya Markert Street Tanga juzi , Diana …

Mke wa Rais Obama Kujadiliana na Wasichana Watanzania

  WASICHANA 25 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kufanya majadiliano ya moja kwa moja na mke wa Rais wa Marekani, Bi Michelle Obama wiki ijayo. Wasichana hao ni miongoni mwa wasichana wa nchi tatu watakaoshiriki majadiliano hayo yenye lengo la kumuwezesha mtoto msichana katika masuala mbalimbali na upatikanaji wa fursa. Majadiliano hayo ni tukio litakalofanywa na Shirika la Plan International Tanzania …

Hofu ya Kimbunga Yazua Taharuki Florida, Marekani

  GAVANA wa Jimbo la Florida nchini Marekani, Rick Scott ametoa tahadhari kuwa uharibifu utakaotokea utakuwa mkubwa sana ikiwa kimbunga Matthew kitapiga maeneo ya jimbo hilo. Bw Scott ametoa wito kwa wakazi wa jimbo hilo kujiandaa kuhama makwao zoezi ambalo ndilo litakalokuwa kubwa zaidi katika historia ya jimbo hilo. Msongamano mkubwa wa magari na watu umetokea katika barabara huku watu …

Watu Wenye Silaha Washambulia ‘Kijiji’ Kenya, Wauwa

  WATU kadha wanahofiwa kufariki dunia baada ya watu wenye silaha kushambulia mtaa mmoja mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya. Taarifa zinasema washambuliaji hao walivamia ploti moja usiku wa manane. Gavana wa jimbo la Mandera Ali Roba ameandika kwenye Twitter kwamba watu 6 wameuawa na mmoja kujeruhiwa. Amesema watu 27 kati ya 33 waliokuwa kwenye ploti hiyo wameokolewa na maafisa …

Magaidi Wavamia Jumba la Starehe Ujerumani, Watu Sita Wauawa

WATU sita wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye bunduki walio wafyatulia risasi watu katika jumba moja la kibiashara mjini Munich, Ujerumani. Taarifa za Polisi zinasema washukiwa bado hawajakamatwa na wamewatahadharisha watu na kuwashauri kutotoka nje. Operesheni kubwa ya kiusalama inaendelea katika jumba la kibiashara la Olympia, ambalo linapatikana mtaa wa Moosach, Kaskazini Magharibi mwa Munich. Watu walioshuhudia tukio wanasema …